Yule
trafiki wakike wa Kenya ambae kwa sasa Wakenya wengi wanamuita Koplo
Linda Okelo ameingia tena kwenye headlines huko huko Kenya na kwa sasa
ameamua kwenda mahakamani kupinga hatua ya kamati ya kinidhamu
iliyowekwa.
Hatua hiyo ni ya kuchunguza madai ya kuvaa sketi fupi ambayo imesemwa
kuwa ilikua nje ya maadili ya kazi na sheria za Jeshi hilo la Polisi la
nchini Kenya.
Kupitia kwa wakili wake Tom ojienda Koplo Lindah amesema kwamba
hakufanya kosa lolote kuvaa sketi hiyo hadi kulazimika kuundwa kamati ya
kumchunguza na kutoa maelekezo ya adhabu anayostahili.
Lindah amesema kwamba asubuhi ya April 26 alifanya mkutana na OCPD
wa kituo cha kiambu ili kuelekezwa,ingawa mkuu huyo wa polisi hakusema
lolote kuhusiana na mavazi aliyovaa.
Ingawa May 2 Lindah alichukuliwa hatua za kinidhamukwa kosa la kuvaa
mavazi yaliyombana kulingana na sheria za huduma za polisi-alivyo kuwa
amevalia sketi fupi iliyombana saa saba mchana nje ya tawi la benki ya
KCB lililopo kiambu.
Linda amedai kwamba sketi iliyo zua utata alikabidhiwa na afisa anaye
shughulika na sare za polisi mwaka 2003 na amekua akivaa kila siku na
mabosi wake hawakuwahi kulalamika kabla ya tarehe 26 Aprili.
Wakili wake Ojienda amesema kwamba wakati wa kikao cha kamati hiyo
may 7 na may 9 Bii Okelo alichukuliwa hatua kimakosa kwani hakukua na
sababu za kumuhukumu kulingana na mavazi yake,kesi yake itatajwa june 12
mwaka huu.
SOURCE: millardayo
Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment