MWANAFUNZI AMBAKA MTOTO WA KAKA YAKE MPAKA KUMVUNJA MGUU..
Jeshi la polisi mkoa wa Mara linamshikilia kijana mmoja ambaye ni
mwanafunzi wa kidato cha 2 katika shule ya sekondari ya Kemoramba
wilayani Butiama, baada ya kutuhumiwa kumbaka mtoto wa kaka yeke
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi, mkazi wa kijiji cha
Nyankanga wilayani Butiama.Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa
Mara ACP Paul Kasabago, amesema kuwa mtoto huyo alibakwa hadi kuvunjwa
mguu wakewa kushoto.Mama mzazi wa mtoto huyo Bi. Annaberi Waitara,
akizungumzia tukio hilo akiwa Hopitali ya Serikali Mkoa wa Mara
Musoma, amesema kuwa mtoto wake alibakwa na Shemeji yake huyo baada ya
kumuachia wakati alipokwenda kuchota maji kisimani
SOURCE: CHINJI THE GREAT
No comments:
Post a Comment