Na Baraka Mbolembole
Senegali ifikia hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia
mwaka 2002 katika nchi za Korea Kusini na Japan na kuwa timu ya pili ya
Afrika kufika hatua hiyo baada ya Cameroon kufanya hivyo mwaka 1990
nchini Italia.
Senegal kama ilivyo kwa Cameroon ilifanya vizuri katika michuano yake ya
kwanza ya fainali hizo kubwa zaidi za soka duniani. Wakati Ghana
ilikuwa timu ya tatu ya Afrika kufika hatua hiyo . Wakicheza fainali za
pili mwaka 2010, Black Stars ilifika hatua ya robo fainali na kuondolewa
kwa changamoto ya mikwaju ya penalty na Uruguay. Saa moja usiku wa leo,
miamba wa soka Afrika wataanza kutupa karata yao ya kwanza kwa
kushuhudia Cameroon wakipambana na timu ya Mexico kutoka Marekani Ya
Kati.
Cameroon ilifuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka
1990 katika fainali ambazo zilifanyika nchini Italia. Cameroon
walipangwa katika kundi moja na waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano
hiyo, Argentina na Romania na Urusi na walimaliza kama vinara wa kundi
baada ya kuifunga Argentina katika mchezo wa ufunguzi kwa goli la
mshambuliaji, Francois Omani Bjyik, wakaicha Romania katika mchezo wa
pili kwa magoli 2-1 ingawa walipoteza dhidi ya Urusi kwa magoli 4-0
katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.
Senegal maarufu kwa jina la `Simba wateranga` walifika robo fainali mwaka 2002.
Wakaichapa
Colombia kwa magoli 2-1 katika mchezo wa hatua ya 16 na kuwa timu ya
kwanza kutoka barani Afrika kufika hatua ya juu zaidi katika michuano
hiyo. Walitinga robo fainali kwa msaada wa mshambiliaji Roger Millar
ambaye alifunga magoli yote mawili akiwa na umri wa miaka 38.
Goli la David Platt katika dakika ya 25 lilifutwa na Emmanuel Kunde
kabla ya Eugene Ekeke kuongeza goli lingine wakati Cameroon ilipotoka
nyuma na kuongoza dhidi ya England katika mchezo war obo fainali. Magoli
hayo yalifungwa katika dakika za 61 na 66 kabla ya Gery Lineker
kusawazisha katika dakika ya 83 na kufanya mchezo huo kwenda katika
hatua ya dakika 30 za nyongeza. Na katika dakika ya 105, England
wakapata mkwaju wa penalty na Lineker akafunga goli la ushindi ambalo
lilihitisha mafanikio ya ‘ Simba Wasioshindika’ katika fainali zao za
kwanza.
Miaka minne iliyofuata nchini Marekani, Cameroon walipangwa katika kundi
la pili sambamba na Brazil, Sweden na Urusi. Walianza na sare ya
kufungana magoli 2-2 na Sweden, wakachapwa magoli 3-0 na Brazil na
wakakutana na kipigo kikubwa zaidi mbele ya Urusi baada ya kutandikwa
magoli 6-1. Walichoambulia katika fainali za mwaka 1994 ni rekodi
iliyowekwa na mshambuliaji, Rogar Millar ambaye alifunga goli la kufutia
machozi la Cameroon akiwa na umri wa miaka 42 na kuweka rekodi ya
mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi iliyodumu hadi sasa.
Kikosi cha Cameroon kilichofika robo fainali mwaka 1990
Cameroon
waliondolewa katika hatua ya makundi wakiwa na pointi moja tu. Walifuzu
kwa mara ya tatu katika fainali za Ufaransa, mwaka 1998 na wakaangukia
katika kundi la pili sambamba na Italia, Chile na Austria. Walitoa sare
dhidi ya Chile na Austria na kuifunga Italia kwa magoli 3-0. Katika
fainali zao za nne katika nchi za Korea Kusini na Japan, 2002 walipangwa
na Ujerumani, Ireland na Saudi Arabia. Walianza michuano kwa sare ya
kufungana goli 1-1 na Ireland wakaishinda Saudi Arabia kwa goli 1-0
lakini wakajikuta wakipoteza mchezo wa mwisho dhidi Ujerumani baada ya
kulazwa magoli 2-0.
Waliishia katika hatua ya makundi kwa mara nyingine. Mabingwa hao wa
zamani wa Afrika walifuzu kwa fainali za Afrika ya Kusini, miaka minne
iliyopita baada ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya mwaka 2006, nchini,
Ujerumani. Walipangwa na Denmark, Japan na Uholanzi. Walifungwa na
Denmark kwa magoli 2-1 wakaishinda Japan kwa goli 1-0 katika mchezo wa
pili kabla ya kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Uholanzi baada ya
kulala kwa magoli 2-1 na wakaishia hatua ya makundi.
Samuel
Eto`o alishangilia kwa staili ya kibabu kinachotembelea mkongojo baada
ya kufunga bao katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani, hii ni
kejeli kwa Jose Mourinho aliyemuita mzee. Leo nyota huyo anaiongoza
Cameroon kombe la dunia.
Kuelekea
mchezo wa jioni ya leo dhidi ya Mexico, kikosi cha Cameroon chini ya
kocha, Voljer Finke kinakabiliwa na changamoto kubwa kuhakikisha
wanapata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa
hatua ya mtoano. Baada ya ushindi wa Brazil dhidi ya Croatia, Cameroon
itakuwa na nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya 16 kama watapata ushindi
jioni ya leo. Ratiba inaonesha watakutana na Croatia katika mchezo wa
pili kabla ya kumaliza na Brazil hivyo ushindi katika mchezo wa leo ni
muhimu sana kama wanataka kufuzu kwa hatua inayofuata. Mshambuliaji,
Samuel Eto’o atakuwa akicheza fainali zake za tatu za kombe la dunia na
nchi yake itakuwa ikicheza fainali za sita. Cameroon wanauzoefu wa
kutosha wanaweza kutinga hatua ya 16 bora wakishinda mchezo wa leo dhidi
ya Mexico.
No comments:
Post a Comment