Breaking News
recent

HATIMAYE BRAZIL YAMTIMUA KOCHA WAO LUIZ FELIPE SCOLARI BAADA YA KUFANYA OVYO KOMBE LA DUNIA..


Rio de Janeiro, Brazil. Chama cha Soka Brazil (CBF) kimesema hakitampatia kocha wa Selecao, Luiz Felipe Scolari, mkataba mpya, vinaripoti vyombo vya habari nchini humo, masaa machache baada ya Ujerumani kutwaa Ubingwa wa Kombe la Dunia kwa mara ya 4.

Scolari, anayefahamika zaidi nchini humo kwa jina la utani la Felipao, alitangaza wiki iliyopita kuwa hataachia hatamu hadi michuano hiyo itakapoisha, akisisitiza kuwa baada ya hapo, ataacha CBF ifanye uamuzi ‘stahiki.’

Taarifa hizi kutoka Rio zilitarajiwa, kwani toka vijana hao wa Manjano waadabishwe 7-1 na Uholanzi kwenye nusu fainali Jumanne ilopita, mashabiki wa ‘futbol’ nchini Brazil wamekuwa wakilia na Felipao wakimtuhumu ‘kulivuruga’ soka lao.

Kwa karibu siku tatu mfululizo, magazeti nchini humo yamekuwa yakianza siku na taarifa zinazomtaka Scolari ‘asepe’, huku gazeti maarufu la kila siku la O Dia likimwambia kocha huyo “aende zake kuzimu.”

Udhaifu uloonyeshwa na Brazil katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia ya 2014 umetonesha kidonda kilichokuwa kimeanza kukauka cha “Maracanazo.”

Dhahama hiyo ya “Maracanazo” Wabrazil wanaikumbuka vyema, kwa jinsi Selecao ilivyoadhirishwa na Uruguay katika fainali ilofanyika uwanja wa Maracano mwaka 1950.

Kabla ya balaa hili la 2014, Scolari alikuwa anafahamika zaidi kwa kuiwezesha Brazil kutwaa Kombe la Dunia kule Japan mwaka 2002.

Kocha huyo mkongwe alikabidhiwa tena mikoba ya Selecao Desemba mwaka juzi, na akafanikiwa kukiwezesha kikosi hicho cha makinda kuchukua Kombe la Ubingwa wa Mabara lilofanyika Brazil mwaka jana.

Kufuatia ushindi huo wa Mabara, kikosi hicho kilitarajiwa kuchukua Kombe la Dunia kwa mara ya 6 lilipochezwa nyumbani mwezi Juni hadi Julai.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya soka hawajawahi kufurahishwa na utendaji wa Felipao, wakidai kuwa staili yake ‘haivutii macho’ kwani inazingatia zaidi uchezaji wa ‘mabavu’
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.