UTANGULIZI
Watu wengi wameielezea mada hii, ila wengi wao wamewekea mkazo
zaidi katika mambo yanayomzuka msomaji kama wakati, utayari, na
kadhalika. mimi nitaweka mkazo katika usomaji wenyewe wa kuelewa na kufaulu.Kitovu chenyewe cha usomaji wa kuelewa na kufaulu ni juu ya kile unachosoma
na si mazingira au wakati unaoutumia kusoma.Kumbuka, tunasoma
vilivyoandikwa na wanadamu na si malaika hivyo si vyote tunavihitaji
bali ni yale mawazo makuu ambayo ndiyo chakula cha fikra zetu.
Hivyo lengo la kusoma ni kuimarisha fikra zetu kwa kuchukua mawazo makuu kutoka kwa mwandishi .fikra ni ule uwezo wetu wa juu wa kufikiria tunaoutumia kuyatazama mambo na kuyapambanua au kuyafafanua.
kifilosofia wengi watakubaliana nami kuwa kusoma ni njia bora sana ya kutafuta mawazo mapya na kuimarisha fikra zetu japo kuna njia nyingi.kwahiyo dhana ya usomaji inakwenda sambamba na kuimarisha fikra zetu kwa kuokota mawazo makuu ya mwandishi na kuyafanya sehemu ya fikra zetu.Kwasababu hiyo tunaepukana na tabia ya kufungasha utitiri wa maelezo akilini kwaajili ya kujibu mitihani tu kama ilivyozoeleka.
Nashukuru kuwa pamoja nami katika utangulizi huu, sasa naomba endelea kupata mawazo mapya ya usomaji wako wa kuelewa na kufaulu.Na hizi ni kanuni kadhaa za usomaji wako:-
(I) TAFUTA MAWAZO MAKUU YA MWANDISI
Hapa ninaomba uwe makini sana, maana msingi wenyewe wa mada hii umeegemea zaidi katika kipengele hiki.
Ninaposema tafuta mawazo makuu ya mwandishi,
nina maana taka kujua kuwa mwandishi anakusudia kuzungumzia nini hasa
au dhima la mwandishi katika mada hiyo. Hii itakusaidia katika
kutochanganywa na maelezo marefu au mtindo atakaokuwa ameutumia
mwandishi katika kuielezea mada husika.Kufanya hivyo kunatokana na
ukweli kuwa wengi hutumia maelezo marefu katika kuwasilisha mawazo.
unapaswa kuwa makini katika usomaji wako wa kuelewa na kufaulu kuhusu swala zima la ubainishaji wa mawazo makuu ya mwandishi, kwasababu hayo ndiyo yanayotakiwa sana na fikra zako
HATUA ZA KUFUATA KATIKA KUBAINISHA MAWAZO MAKUU YA MWANDISHI
(A) ELEWA KILA SENTENSI IKIWEZEKANA KILA NENO
Hii itakusaidia katika kubaini mawazo makuu bila
kuwa na shaka ya kile ulichosoma .Wengi wametumbukia katika mtego wa
kutoelewa maana ya kile walichosoma na kujikuta wakitumia nguvu nyingi
kusoma lakini hakuna wazo jipya linaloingia akilini.Tatizo hili
linatokanana na kutoelewa kilichozungumzwa na mwandishi. Hapa
panahusisha nyenzo mbalimbali ikiwemo kamusi nk. kama nitakavyofafanua
katika kipengele cha (VII)
(B) PIMA UELEWA WAKO JUU YA MADA ULIYOISOMA
Mara baada ya kumaliza kusoma mada moja funga ukurasa wako na kujiuliza swali moja tu, kwamba mada ilizungumzia nini? hapa unaweza kuelezea katika ufahamu au katika karatasi uliyoiandaa tena katika lugha uliyoizoea .
Andika ulichojifunza katika mada hiyo kwa ufupi kisha fungua tena ukurasa kwa lengo la kujiridhisha kama uko pamoja na mwandishi.Hapa utaona umakini umeongezeka kwa sababu ya kutaka kujua wapi ulikosea katika kujieleza kwako. Hivyo hautakuwa mgeni tena katika mada hiyo na utakuwa tayari kwa hatua inayofuata .
Andika ulichojifunza katika mada hiyo kwa ufupi kisha fungua tena ukurasa kwa lengo la kujiridhisha kama uko pamoja na mwandishi.Hapa utaona umakini umeongezeka kwa sababu ya kutaka kujua wapi ulikosea katika kujieleza kwako. Hivyo hautakuwa mgeni tena katika mada hiyo na utakuwa tayari kwa hatua inayofuata .
Kumbuka wengi huishia hatua hii na kukimbilia maswali
bila kuingia hatua inayofuata ambayo ndiyo muhimu kuliko kujibu maswali.
Elewa, maswali huishia shuleni tu lakini fikra zetu tunaishi nazo siku zote .
Kwasababu hiyo zingatia kubaki na mawazo mapya katika fikra zako kuliko
kutumia mawazo hayo kwa muda tu katika kujibu maswali.
(C) ORODHESHA MAWAZO MAKUU YOTE YA MWANDISHI NA KUELEZEA KWA
MANENO YAKO
Hii ndiyo hatua muhimu na ya pekee kabisa katika kupakia mawazo mapya katika usomaji wako wa kuelewa na kufaulu .Panga mawazo makuu uliyoyaona katika mada kama unavyoona katika mfano wa mada moja inayohusu ukimwi:-
*maana ya ukimwi
*maambukizi ya ukimwi
*kinga ya ukimwi
Tufanye
haya ndiyo mawazo makuu uliyoyaona katika mada moja ndeefu inayohusu
ukiwi.Hapo ndipo uanze kuilezea mada hiyo kwa ufasaha kwa maneno yako
ukitumia lugha ya mwandishi kama unaimudu.Hakikisha kuwa katika maelezo
yako unaepuka kwenda mbali na maana ya maneno yaliyotumika katika mada
hiyo.Tumia mawazo yote makuu uliyoyapata katika mada ukianzia na wazo la
kwanza hata la mwisho bila kurudi kwa mwandishi.Hakiki kwa mara ya
mwisho kama umeweza kuchukua mawazo yote ya muhimu na kama la,tulia kwa muda kisha sahihisha makosa.
Kitendo hicho kitaifanya mada hiyo kuwa yako na si
ya mwandishi tena; tayari imesha hamia akilini mwako na hivyo sasa uko
tayari kwa maswali au kuiwasilisha popote utakapotakiwa.Huu ndio
unaoitwa usomaji wa kuelewa na kufaulu yaani fikra zako
zimebadilika na unaweza kuwa na mchango katika mada husika.Kumbuka, sasa
akilini mwako mada haijafungashwa kama mzigo bali mada hiyo ni sehemu ya fikra zako. kwasababu hiyo sasa unauwezo wa kuelezea kuhusu ukimwi ,tabia nchi,mfumo wa mmeng'enyo nk,kwa maneno yako na si ya mwandishi tena.
(II) SOMA MADA MOJA KWA WAKATI
Usomaji wa kuchanganya mada unaweza kukufanya
uchanganye mawazo au kutokuhifadhi mawazo mapya kwa usahihi.Vilevile
kunaweza kufanya mada hizo kutokuwa sehemu ya fikra zako bali mzigo
unaoweza kukudondoka wakati wowote. Kwasababu hiyo kuwa na mada moja
kwa wakati ni njia bora zaidi kwa usomaji wenye tija .
(III) PITIA NOTES AMBAZO UMEZIANDAA MWENYEWE
Kupitia notes ambazo umeziandaa mwenyewe ni vyema sana kwasababu itakusaidia kukumbuka kwa urahisi mada uliyokusudia kuisoma.Wengi tunapenda mteremko katika kusoma kwa kuchukua notes za watu wengine au vitabu bila kuvibadililisha kuwa fikra zetu.Kitendo
hicho kinatufanya kupata ugumu wa kukumbuka katika usomaji
wetu.Kwasababu hiyo usikubali kupoteza muda mwingi katika kulazimisha
fikra za watu wengine kuingia akilini mwako, bila kuzipanga upya kwa
namna unayoweza kuzihifadhi akilini mwako kirahisi.
(Iv) PITIA NA WAANDISHI WENGINE WALIOZUNGUMZIA MADA HIYO
Sasa ukiwa na uzoefu wa mada uliyoisoma unaweza kupitia na waandishi wengine waliozungumzia mada uliyosoma ukiwa na mchango flani katika mada husika .
Hii itakusaidia kupata uzoefu wa kuelezea au kuifanyia utafiti mada husika katika mitazamo au namna tofautitofauti.
(V) HESHIMU MUDA UNAOUTUMIA KUSOMA
Mimi sio muumini wa wakati gani wa kusoma maana
wakati unategemeana na ratiba ya mtu. kuna wanaosema wakati mzuri ni saa
mbili mpaka saa nne usiku, kuna wanaosema wakati mzuri ni saa kumi
alfajiri hadi saa nne asubuhi na wanasababu zao. Lakini mimi ninaamini
mtu anaweza kusoma wakati wowote ilimradi asiwe amechoka sana.
unachotakiwa kufanya ni kutoshughurika na jambo lolote nje ya kile unachosoma.Miongoni mwa mambo hayo ni:- kuchati ,kuzungumza ,kusikiliza taarifa ya habari au midundo na kutazama runinga .Hii itakupelekea kupoteza sehemu kubwa ya mawazo mapya kwa kugawa fikra zako kutafakari kinachoendela nje ya mada. Hivyo kukufanya wakati wa ubainishaji wa mawazo makuu kuwa na kumbukumbu hafifu kuliko kama ungejishughulisha na jambo moja.
(VI) EPUKA KUKESHA
Usomaji wa kukesha ni wa mbwembwe unaotokana na
dhana potofu ya wasomi wa kizamani.Baadhi yao wanaodai kuwa walikuwa
wakiweka miguu kwenye maji usiku kucha ili wapate kusoma sana .Mkumbo
huu unaweza kuvuruga kabisa uelewa wako. Kwasababu hutakuwa na nafasi ya kubainisha mawazo makuu kutokana na kuwa na utitiri wa mada nyingi zinazosomwa kwa wakati mmoja.Zaidi ya yote hutakuwa na nafasi ya kubadili mawazo hayo kuwa fikra zako.
(VII) TUMIA NYENZO SAHIHI KATIKA USOMAJI WAKO
Hapa panahusisha nyezo kadhaa zinazofanya usomaji usiwe mzigo.Maana yake ni kuwa usome ukistarehe.
Zifuatazo ni baadhi ya nyenzo muhimu katika usomaji wa kuelewa na kiufaulu.
Zifuatazo ni baadhi ya nyenzo muhimu katika usomaji wa kuelewa na kiufaulu.
computer .
Unaweza kutafuta computer ambayo utaingiza baadhi ya programu kama ADOBE READER , E-BOOK READER ,PDF SUITE,PDF CREATER kwaajili
ya kusomea.Pia unaweza kutumia programu hizi kubadilisha format ya
mafaili yako na wakati mwingine kuyahifadhi katika mtandao.Unaweza
kutumia Adobe acrobat ambapo kupitia adobe acrobat account
unaweza kuhifadhi faili za notes zako katika mtandao.Hata hivyo kuna
huduma ya google drive ambayo ni bure unayoweza kuitumia kuhifadhi
mafaili yako kupitia account yako ya google mail.
Faida utakayoipata ni kama endapo notes zako zitapotea au kuibiwa au kuharibika kwa namna yeyote ile ,bado utakuwa na uwezo wa kuzipata bila shida tena kwa kutumia hata simu ya mkononi.Utakuwa na nafasi ya download na kuzihifadhi upya Tena kama adobe reader ni programu ambayo ikiwezeshwa inaweza kusoma kwa sauti notes zako na wewe kubaki msikilizaji.kujua kiundani jinsi ya kuitumia huduma hii bofya hapa Jinsi ya kusoma kwa kusikiliza ukitumia ADOBE READER.
Faida utakayoipata ni kama endapo notes zako zitapotea au kuibiwa au kuharibika kwa namna yeyote ile ,bado utakuwa na uwezo wa kuzipata bila shida tena kwa kutumia hata simu ya mkononi.Utakuwa na nafasi ya download na kuzihifadhi upya Tena kama adobe reader ni programu ambayo ikiwezeshwa inaweza kusoma kwa sauti notes zako na wewe kubaki msikilizaji.kujua kiundani jinsi ya kuitumia huduma hii bofya hapa Jinsi ya kusoma kwa kusikiliza ukitumia ADOBE READER.
pia unaweza ku install kamusi mbalimbali katika computer
yako kwa mahitaji yako.Waweza pia kutumia programu nyingine kama microsoft office
ambayo imekuwa na sifa nyingi za kumfanya msomaji asiwe na tabu katika
usomaji. Tukipata nafasi tutatazama kwa undani jinsi tunavyoweza kutumia
programu hii katika usomaji wetu.
kwa kutumia computer pia unaweza ku share na marafiki
notes na maswali bila kupoteza muda kwa kutumia nyenzo mbalimbali
zilizomo humo mfano (home group network) nk.
endapo utapata matatizo ya kupararaizi au kuumia mikono,
kwa kutumia computer unaweza kuendelea kusoma, kuchukua notes ,na
mengine kupitia speech recognition application na
nyinginezo. Utabadili baadhi ya command katika computer yako ili iweze
kutambua lafudhi yako na utaitumia bila shida. Mimi nimejaribu inafanya
kazi .
kipengele hiki kinahitaji somo ili kiweze kukaa sawa. Tukipata nafasi tutaliweka sawa
FLASH,CDS
Hivi
ni vifaa vinavyoweza kubeba kumbukumbu za kielectronic za kimaandishi
na picha kwa kiasi kikubwa kulingana na uwezo wa kifaa chako .unaweza
kubeba kurasa za usomaji wako wa mwaka mzima kwenye kifaa kimoja.Inakupa urahisi wa kukitumia mahala popote penye computer au kifaa chenye uwezo wa kusoma kilichomo ndani ya cd au flash yako.
Angalizo:
vifaa hivi huwa vikiharibika huwa havina uwezo wa kuonyesha hizo data
zilizomo ndani yake, hivyo ni muhimu kuwa na nakala katika kila
unachohifadhi kwenye vifaa hivyo.
SIMU (TABITI) TABLETS
Nyingi ya hizi tabiti au vifaa simu vinauwezo wa kutusaidia katika masomo hasa tunapokuwa mbali na nyumbani.unachoweza
kufanya, kama simu yako sio ya window au ni android, ni ku download
application program mbalimbali zinazoweza kufanyakazi kwenye simu yako.
Tafuta aplication zenye uwezo wa kufungua mafail yenye format ya pdf na xps, ambayo utakuwa umeyahifadhi kwenye phone memory au kwenye memory iliyopachikwa kwenye simu yako na hata yale uliyoyahifadhi kwenye mtandao.
Tafuta aplication zenye uwezo wa kufungua mafail yenye format ya pdf na xps, ambayo utakuwa umeyahifadhi kwenye phone memory au kwenye memory iliyopachikwa kwenye simu yako na hata yale uliyoyahifadhi kwenye mtandao.
baadhi ya application zinazofanya vyema kwenye android phone kufungua mafaili ya format ya pdf na xps ni android pdf viewer,quickoffice na e-book droid. Pia
unaweza ku download application nyingine kama online
dictonary,wikipedia na nyinginezo ambazo zinaweza kukusaidia tafsiri ya
maneno unapokuwa peke yako.
kamusi
Nimuhimu
sana kwa mtu mwenye nia ya dhati kusoma kwa kuelewa na kufaulu kuwa na
zana hii na nyingine zinazo fanana na hiyo kulingana na
unachosoma.kamusi zitakusaidia kutafsiri maneno mapya kwako yaliyotumiwa na mwandishi kuliko kutegemea kuuliza kila kitu kwa watu ambao pengine wasikusaidie kwa wakati.
kwakutumia mwongozo huu wa kusoma wa kuelewa na kufaulu nina imani utakuwa umenufaika vya kutosha hivyo utaachana na usomaji wa kimazoea usikokuwa na tija .
No comments:
Post a Comment