Beyonce Knowles, ameongoza nafasi ya kwanza katika list ya watu 100 maarufu duniani kwa mujibu wa Forbes
Forbes wamefanikiwa kutengeneza list hiyo baada ya kufatilia mkwanja walioingiza tangu June 2013 mpaka June 2014 na pia umaarufu wa watu hao kupitia mitandao ya kijamii, radio pamoja na television kujua ni mara ngapi wamekuwa wakitajwa.
Beyonce amemtoa Oprah kutoka katika nafasi hiyo ya kwanza ambayo aliishika mwaka jana, na kumpeleka mpaka nafasi ya nne mwaka huu, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na mcheza kikapu Lebron James.
Beyonce pia ameachia album yake mpya "Beyonce" December bila promo yoyote, single "Drunk in love" tayari mpaka sasa imeshauza zaidi ya kupi milioni moja.
Nafasi ya 2 imeshikiliwa na mcheza kikapu Lebron James, 3 ni Dr Dre, nafasi ya 4 imeshikiliwa na Oprah Winfrey, Nafasi ya 5 imechukuliwa na Mtangazaji Ellen Degeneres, huku Jay Z akiwa ameshika nafasi ya 6
Mshkaji wa karibu na 50 Cent, Floyd Mayweather Jr ameshika nafasi ya saba, huku Rihanna akiwa nafasi ya 8, Katy Perry amekamata nafasi ya 9 huku ya kumi ikiwa imehukuliwa na Robert Downey Jr muigizaji wa movie ambae mkwanja mwingi ameingiza mwaka huu kupitia "The Irone Man 3"
No comments:
Post a Comment