Kampuni moja ya Florida, Marekani imekuja na dhana ya kujenga meli ‘Freedom Ship’,itakayokuwa na uwezo wa kuwa na kila kitu cha kuifanya iwe jiji linaloelea kwenye maji.
Wabunifu wa dhana ya meli hiyo wametoa picha za computer za kile wanachoamini meli hiyo itakavyokuwa pindi itakapokamilika.
Roger M Gooch, mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni ya Freedom Ship International ya Florida, Marekani, ambao ndio wenye mradi huo, amesema hiyo itakuwa ndio meli kubwa kuwahi kujengwa, na jiji la kwanza linaloelea kwenye maji. ‘The Freedom Ship will be the largest vessel ever built, and the first ever floating city.’
Uwanja wa ndege utakaokuwa juu ya meli itakayowezesha ndege kuruka na kutua hata wakati meli inatembea
Gooch, Amesema kampuni yake inajaribu kukusanya kiasi cha £6 billion zinazohitajika kuifanya ndoto hiyo iwe kweli, ambayo mpango wake umekuwepo kwa miaka mingi.
“But in the last six months we’ve been getting more interest in the project and we are hopeful we will raise the $1billion (£600million) to begin construction.’ The ship would spend 70 per cent of its time anchored off major cities and the rest sailing between countries” Aliongeza.
Freedom Ship, itakuwa na huduma zote za jiji kama Shopping center, shule, hospitali, uwanja wa ndege, casino, parks nk.
Meli hiyo inayotegemewa kuwa na ghorofa 25, itakuwa na uwezo wa kuwapa makazi ya kudumu watu 50,000, lakini itakuwa na nafasi ya ziada ya kupokea wageni wengine 30,000, makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa usiku mmoja.
Hii ndio njia inayotarajiwa kutumiwa na meli hiyo kuizunguka dunia
Meli hiyo inatazamiwa kuwa inazunguka dunia nzima nchi moja hadi nyingine, bara moja hadi linge na itafika hadi Afrika, na haitakuwa ikikaa sehemu moja kwa muda mrefu.
Itakuwa na makazi ya watu 50,000 pamoja na makazi ya wageni 30,000 na makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa usiku mmoja.
Meli hiyo itakuwa na huduma zote za muhimu zinazopatikana katika majiji mbalimbali zikiwemo hospitali, shule, maduka, parks, casino, aquarium, kiwanja cha ndege chenye njia ya kuruka na kutua ndege ndogo zenye uwezo wa kubeba watu 40, kitakachokuwa juu kabisa kwenye paa la meli hiyo.
Meli hiyo itakuwa ikitumia umeme wa solar pamoja na wave energy.
Itakapokamilika, jiji linaloelea litakuwa na upana wa 750ft, urefu wa kwenda juu350 ft, pamoja na urefu wa 4,500 ikiwa ni mara nne ya Queen Mary II Cruise ship iliyokuwa na urefu wa 1,132ft.
Wageni na wenyeji wanauwezo wa kuondoka na kuingia kwenye jiji hilo la majini kwa ndege au boti
No comments:
Post a Comment