UEFA
Jana ilitoa Majina 10 ya Wagombea Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka na
Mshindi {atatangazwa hapo Agosti 28 wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI.
Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na hao 10 ndio kuibuka kidedea.
Lakini
Majina hayo 10 yatachujwa kwa Kura hapo Agosti 14 na kubakisha Majina
Matatu yatakayopigiwa Kura na kutangazwa Mshindi hapo Agosti 28.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Miongoni mwa Majina makubwa ambayo hayamo kwenye Listi hii ya Wachezaji 10 ni yale ya Zlatan Ibrahimovic, Gareth Bale na Neymar.
Lakini
yapo Majina ya Wachezaji Watatu toka Kikosi kilichochukua Kombe la
Dunia cha Germany Jumapili iliyopita huko Brazil na pia yupo James
Rodriguez alietwaa Buti ya Dhahabu huko Brazil kwa kuwa Mfungaji Bora wa
Kombe la Dunia akiichezea Nchi yake Colombia.
Bila kustajabisha, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa Wagombea.
Tuzo
hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or
ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia
kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa
Klabu.
LISTI YA WAGOMBEA 10:
-Diego Costa [Spain, Atletico Madrid]
-Angel Di Maria [Argentna, Real Madrid]
-James Rodriguez [Colombia, AS Monaco]
-Luis Suarez [Liverpool (Sasa Barcelona), Uruguay]
-Philipp Lahm [Germany, Bayern Munich]
-Thomas Muller [Germany, Bayern Munich]
-Manuel Neuer [Germany, Bayern, Munich]
-Arjen Robben [Germany, Bayern Munich]
-Cristiano Ronaldo [Portugal, Real Madrid]
-Lionel Messi [Argentina, Barcelona]
WACHEZAJI 25 WALIOBWAGWA TOKA LISTI YA WACHEZAJI 35:
**Namba ni Nafasi waliyoshika kwenye Kura
No comments:
Post a Comment