Well the champ is ..... you know,hatimaye ndoto ya John Cena kuwa Wwe Heavyweight champion imetimia,hii ni baada ya kupambana na miamba nane katika ulingo mmoja hapo jumapili huko marekani.
Cena ambaye sio mchezaji mzuri sana katika mapigano ya kutumia ngazi,alionesha uwezo wake pasipo watu kutegemea na kupambana hadi mwisho na kuhakikisha anatoka na ubingwa na ndivyo ilivyokuwa kwa upande wake.
Mechi ilianza baada ya miamba nane kuingia uwanjani hapa nawazungumzia John Cena,Randy Orton,Roman Reigns,Alberto Del Rio,Sheamus,Kane,Antonio Cessaro pamoja na Bray Wyatt,Sheamus ndiye aliyekuwa wakwanza kupanda ngazi nakutaka kuichuka mikanda hiyo miwili lakinihaikuwa bahati yake kwani wapiganaji wenzake walikuwa wananguvu bado.
Mechi ilikuwa ngumu mno na kupelekea wengine kupata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.Randy Orton aliumia sehemu kichwani baada ya kushushiwa kichapo na mbabe Roman Reigns.
Triple H na mkewe ambaye ni mkuu wa kitengo cha operesheni walikuwa wameketi pembezoni mwa ulingo kushuhudia mechi hiyo,wapiganaji walipambana kwa nguvu zote na kuifanya mechi hiyo kuingia kwenye rekodi za mechi kali za WWE.
No comments:
Post a Comment