Mwanajeshi wa wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi akikabidhi mojawapo ya
vifaa vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia MH17
iliyolipuliwa kwa maofisa wa Malaysia.
Vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia vilivyokabidhiwa.
Mtaalamu wa Malaysia akikagua moja ya vifaa hivyo.
Vifaa hivyo vikiwekwa kwenye mfuko baada ya makabidhiano.
HATIMAYE wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi wamekabidhi vifaa viwili vya
kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege MH17 ya Malaysia
iliyolipuliwa kwa maofisa uchunguzi wa Malaysia huko Ukraine.
Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa ni baada ya wito mbalimbali kutolewa
kuhusu maofisa wa uchunguzi kuruhusiwa kufanya uchunguzi wao eneo hilo
la ajali iliyouwa watu 298.
Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak ameeleza kuwa vifaa hivyo
vilikabidhiwa mjini Donetsk jana baada ya mazungumzo ya muda mrefu na
wapiganaji hao.
Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment