Breaking News
recent

GERMANY IMETINGA FAINALI BAADA YA KUITANDIKA BRAZIL 7 KWA 1.....


Ujerumandiyo timu ya kwanza kufuzu kwenye Fainali ya kombe la dunia Brazil 2014, baada ya kuinyeshea wenyeji Brazil mabao 7-1 katika uwanja wa Estadio Mineirao ulioko Belo Horizonte.
Umakini wa vijana wa Joachim Low ulikuwa wa kupigiwa mfano walipoiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la dunia.

article-2685267-1F7DC01800000578-918_634x637
Kabla ya mechi hiyo vyombo vya habari vilikuwa vimemulika mfumo wake Luiz Felipe Scolari vikidai alikuwa ameumba timu yake kumtegemea Neymar.
Kujeruhiwa kwa Neymar Ijumaa iliyopita ilimlazimu Scolari kubadili mfumo ambao sasa haukuwa na nyota huyo.
Je Scolari atasingizia nini ?

Ilikuwa wazi tofauti ya mbinu za makocha hao wawili wajerumani walipoanza kwa kuwashirikisha washambulizi Miroslav Klose,Thomas Muller na Mesut Ozil huku Schweinsteigerakiwaongoza Toni Krooos Khedira na Lahm katika kiungo cha Kati.
Na Baada ya nipe nikupe ya kufungua mechi Iliwachukuwa Wajerumani takriban dakika kumi tu za kwanza kupenya safu ya ulinzi ya Brazil iliyokuwa inakosa uzoefu wa Thiago Silva.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.