Kwa
kifupi naweza kusema kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu wa nini
kuhusu wewe.Hali yako,umuhimu wako,malengo yako,hatima yako, changamoto
zako, nk, hayo yote yanakuwa wazi kwako kwa kujitambua.
Dhana
ya kujitambua kwa zama za sasa imekuwa kama kengele ya kanisa au azana
ya msikiti, kwa jinsi ambavyo hutamkwa mara kwa mara.Sasa yatosha kwa
jinsi tulivyoisikia,leo nataka tuje na kitu kipya kama kilivyoelezwa
katika kichwa cha mada yetu.
Sipendi kukuchukulia muda wako naomba niingie moja kwa moja kwenye mada
1. PIMA UMRI NA KIWANGO CHA FIKRA ZAKO
Sote
tunafahamu kuwa hakuna kiwango maalumu cha kufikiri kilichoidhinishwa
kimataifa kutoka umri mmoja na mwingine. Bali tunaviwango vya kimataifa
vinavyotoa uwiano wa umri wa mtoto na kuandikishwa shule.Hata hivyo kuna
uwezekano mkubwa wa kupima kiwango cha fikra zako kwa kulinganisha na
umri wako.
Unaweza
kupima fikra zako kwa kutazama ubora wa matokeo ya kila unachoamua
kutenda pasipo kusaidiwa na mtu mwingine.Pia unaweza kupima fikra zako
kwa kuzilinganisha na ubora wa fikra za watu wenye kiwango cha juu cha
fikra katika umri wako. Lakini mwisho wa yote viwango bora kabisa vya
kifikra vinalenga juu ya usahii wa wakati katika kutekeleza jambo
fulani.
Unaweza
kupima jinsi unavyopanga,unavyoamua,unavyotekeleza, na kuendelea au
kusitisha maswala fulani fulani katika maisha yako na aina ya matokeo
unayoyapata kwa kuzingatia ubora wake.
Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuanza kupata picha ya namna gani unajitambua.
2. TAFUTA KUJUA UPEKEE ULIONAO
Hii
nayo ni kati ya mbinu bora inayokufanya ujitambue.Watu wengi hupenda
kufanana na watu fulani fulani haswa watu ambao wao huwaita role model
(mtu wa mfano),Na kusahau kuwa yeye ndiye role model na.1 kwake
binafsi.Makosa haya humpelekea mtu huyo kujua zaidi kuhusu huyo role
model na.2 na upekee wake kuliko anavyoweza kujifahamu mwenyewe.
Leo
imekuwa ni kawaida kumsikia mtu akieleza kwa ufasaa upekee alionao
OBAMA na MKEWE lakini ukimuuliza upekee alionao akakujibu kirahisi tuu
sijui.Kitu pekee kitakachokuokoa na tatizo hili ni kuamua kufahamu
upekee ulionao na si upekee wa mtu mwingine au Role model wako.
Kama
wewe ni mwandishi wa vitabu jiulize unatofautiana nini na waandishi
wengine,au kama ni mwanafunzi,mwanasayansi,mchezaji,mwanajamii, nk,
unatofauti gani na wengine ukiwa na maana uthamani wako uko wapi zaidi.
3. TAFUTA KUJUA CHANGAMOTO ZINAZOKUKABILI
Kama
kweli umedhamiria kujitambua unatakiwa kufahamu changamoto au matatizo
yanayokukabili.Changamoto hizo zinaweza kuwa ni zile zinazotokana na
rika ,mazingira ,kiwango cha elimu yako,Hali uliyonayo (ulemavu,
mahitaji maalumu au uathirika wa magonjwa,ndoa,bila ndoasingle nk. ).
Kama
ni rika tambua rika lako linakabiliwa na changamoto zipi.Ikiwa ni
mazingira tafuta kujua changamoto za kimazingira ulizonazo.Unaishi
kijijini ,mjini,shuleni,chuoni,mfanyakazi,kiongozi,mfuasi au vinginevyo
,jiulize katika mazingira hayo unakabiliwa na changamoto gani.
Inawezekana wewe ni teenager (13-19 miaka) au kijana au mzee, jiulize
kuhusu changamoto zako.Vivyo hivyo kwa kiwango cha elimu pamoja na hali
kama ilivyofafanuliwa katika mabano.Orodhesha changamoto
zinazokukabili.
Kumbuka
hata uonevu wa kibinadamu wa kawaida hutokea zaidi kwa watu
wasiozingatia kipengele hiki cha ufahamu wa changamoto. Hakikisha
unafahamu wapi utakwama kabla hujafikia na kuanza kuchukua hatua mapema
iwezekanavyo.kitendo hicho kitakufanya uwe macho saa zote na kila
atakayekuona atakuthamini hivyo kutokuwa na madhara kwako.
4. TAFUTA KUJUA WAJIBU NA MAJUKUMU YA WATU WA RIKA LAKO
Kwa
haraka unaweza kufikiri kuwa nataka kufundisha uraia.Utanisamehe kama
nitakuwa nimekukumbusha kitu unachoimba au ulichoimba kilasiku
shuleni.Lengo langu nataka nikufumbue macho kuhusu wajibu na majukumu
kama dhana muhimu katika kujitambua.
Mfano;
mama mmoja alikuwa akilia kwa uchungu nje ya nyumba yake huku
akijitupatupa chini na kugalagala.Majirani wakaja mbio na kukusanyika
kufahamu kilichotokea.Lakini kila walipomuuliza mama alichokua akililia
aliwaonyesha kidole katika mlango uliokuwa wazi.
Watu
wakakimbilia ndani na kumkuta mtoto wa miaka minne na nusu aliyewekewa
kila kikorokoro cha kuchezea lakini hakuna alichokishika wala
kukichezea. Walipotoka na kumuuliza mama mbona hatukuona chochote zaidi
ya mtoto na vitu,mama akaongeza kilio na kusema “masikini mwanangu asala
gani hii! huyu ni mwanangu watatu ,wenzake waliotangulia walikufa kwa
moto shambani kwasababu hawakuweza kusogea hata hatua moja moto
ulipotokea nilipokuwa kisimani kuteka maji.kinachoniumiza zaidi ni kuona
hata huyu naye hagusi chochote nilichomwekea nahisi naye atakufa kifo
kama cha wenzake”.
Kwa
mfano huo tunapata picha ya mtu asiyetambua wajibu wake anavyoweza
kuleta hasara kubwa kwake yeye mwenyewe ,kwa familia yake na kwa taifa
lake.Mama aligundua kuwa mtoto wake hajitambui kwa kutonyanyua
chochote.majukumu ya msingi ya mtoto wa umri ule ni kucheza.Kutokucheza
ilikuwa ni ishara tosha ya kutokujitambua.
Jiulize kama wewe ni mmoja wa wale wasiowajibika?.
Piga picha na kuyatazama majukumu yako kama mtoto,kijana,au mzee.
Jiulize kuwa wewe ni Yule mtoto mwenye kila kilicho mbele yake lakini hakuna anachogusa?.
Jiulize kuwa umekuwa mtu wa kunyooshea vidole majukumu au umekuwa mstari wa mbele kutumikia?.
Umewahi kushiriki kutatua kero yeyote nyumbani kwako ,mtaani kwako au maeneo yaliyokuzunguka?
Jiulize unafanya nini katika kujiandaa kutumia fursa zinazojitokeza duniani?
Nafasi uliyonayo unaitumia kufanya wengine kuinuka au unawadidimiza?
Jiulize kama wewe ukikosekana duniani, dunia itakuwa imepata hasara yeyote?
Wakati
unajiuliza maswali hayo ni wazi kuwa utaanza kupata picha ya jinsi
ulivyo kwa kupima uwajibikaji wako.Kitendo kicho kitakufanya uongeze
uelewa wako juu yako binafsi na kwasababu hiyo utaingia kwenye kundi la
watu wanaojitambua.
5. PIMA KUJIAMINI KWAKO
Ili
kujitambua inakupasa kuchukua jukumu hili msingi la kupima kujiamini
kwako.Hebu jichukue katika fikra zako na kujiweka mbele ya umati mkubwa
wa watu wenye uelewa wa kutosha.Jaribu kuwaelezea au kuonyesha kitu
ambacho unakifahamu kwa usahihi kabisa hapa duniani.Unahisi unaweza
kukifanya kikamilifu bila hofu wala kubabaika.
Unaweza kujikumbusha mambo ambayo yalikuwa yanakufanya ushindwe kujiamini kama bado yapo au la.
Pima ubora wa unachofanya kama una nafasi yeyote katika viwango vya kidunia?.
Kama wewe unajihusisha na sanaa je sanaa yako inaweza kumvutia mtu yeyote duniani?.
kama ni huduma je! huduma yako inaweza kumfaa mtu yeyote duniani?
Kama ni mwanafunzi je wewe unaweza kuwa mwanafunzi bora popote duniani au ni hapo kijijini kwako tu?.
Unaweza kushindanishwa na mtu yeyote duniani kwa hilo ambalo wewe ni bora sana hapo kwenu au ubora huo ni wa hapo kwenu tu?.
Kwa vipimo hivyo vitakufanya uzidi kujitambua na kuchukua hatua ya kuondosha mapungufu uliyonayo na kukufanya uzidi kujiamini.
6. WEKA VIPINDI MAALUMU VYA KUJITATHIMINI
Kitendo
cha kujitathimini kitakufanya kujichunguza na kujiweka karibu na wewe
binafsi.Tatizo kubwa tulilonalo leo duniani ni kwamba tunawatu wengi
ambao wako karibu sana na watu wengine lakini hawako karibu na wao
wenyewe. Kifupi ni kwamba wanajua sana kinachoendelea kwa watu wengine
kuliko kinachoendelea kwao binafsi.
Wanalaumu watu hawana elimu wakati wenyewe hawana,
Wanatetea unyanyasaji wa kijinsia wakati wao wenyewe wananyanyaswa,
Wanalaumu watu wanaovunja ndoa wakati wao wenyewe wana nyumba ndogo,
Wanalaumu kuhusu wizi wa viongozi wa umma wakati Wao mwenyewe wanaiba kwenye kampuni zao.
Sasa,kitu
ambacho kinaweza kusaidia katika kujitambua ni kufanya tathmini
binafsi juu ya mwenendo wako.Kabla hatujaanza kukosoa uzembe wa watu
wengine tenga vipindi maalumu ikiwa ni kila baada ya wiki,mwezi au mwaka
kutathimini ni uzembe wa namna gani umefanya na matokeo yake.Hata hivyo
unaweza kufanya tathimini za kila siku ili kutokuwa na mlundikoano wa
tafakuri za muda mrefu kuhusu namna ulivyoishi.
Unaweza
kutathimini kiwango cha mafanikio kwa kulinganisha na matarajio,kiwango
cha mapungufu kwa kwa kulinganisha na namna ulivyoshindwa.Kama
mafanikio hayakufikia malengo basi ni wazi kuwa bidii na mbinu bora
zaidi zinahitajika na kama matokeo ni kushindwa basi ni wazi kuwa mfumo
mzima wa maisha inabidi ubadilike na mbinu mpya zinatakiwa.
Kiwango
cha kujitambua kinaendana na tathimini binafsi. Ni kiwango cha hali ya
juu cha kutojitambua kuendelea na kazi ileile au mbinu ileile
inayokufanya kilasiku ushindwe kutimiza malengo yako.Kila baada ya
tathimini lazima uje na mapendekezo mapya yenye mbinu mpya ,mikakati
mipya na matarajio mapya.Kwa kufanya hivyo ni dhahili kuwa kiwango chako
cha kujitambua kitakua na kuongeza mabadiliko ya kila siku katika
maisha yako.
7. KUBALI KUANZA UPYA
Bila
kujali wasifu ulionao unaweza kuonyesha kiwango cha kujitambua kwako
kwa kuanza upya mara tu unapobaini kuwa kunamakosa makubwa katika
mwenendo wa maisha yako.mtu mwenye kiwango cha chini kabisa cha
kujitambua hawezi kuanza upya .kwasababu ya kutojitambua kwake haoni
shida kwa lolote limpatalo na kuhisi kuwa amestahili.
Mtu
asiyejitambua haoni umuhimu wa kubadilisha mtindo wa maisha kwasababu
hufikiri kuwa kufanya hivyo ni sawa na kupoteza wakati.Inashangaza sana
kumwona mtu anatumia staili ya aina moja katika kupambana na changamoto
ambazo kila siku zinabadilika.
Jenga
tabia ya kukubali kuanza upya kila unapoona kuwa hatua ya kiwango cha
makosa ulichofikia hakiwezi kurekebishika.mfano ,kama pengine fani
unayoitumikia haiendani kabisa na kipaji ulichonacho kubali kuanza
kujifunza fani nyingine.Na endapo marafiki ulionao wanakusababisha
kushindwa kutimiza majukumu yako, kubali kuanza kutafuta marafiki wapya.
Kitendo
cha kukubali kuanza upya kitakufanya kujitambua. Utakapoanza awamu ya
pili itakusaidia kubaini makosa uliyoyafanya mwanzo na kwasababu hiyo
kuwa mwalimu wa wengine.
Kupitia
mada hii bila shaka utakuwa umepata uelewa mkubwa sana kuhusu mbinu ya
kujitambua na sasa unaweza kuwa na mchango mkubwa kwako na kwa jamii
yako.
No comments:
Post a Comment