KLABU ya Besiktas ya
Uturuki imethibitisha kuwa Chelsea imepanga kumuuza mshambuliaji wake
Demba Ba. Toka alipojiunga na Chelsea katika kipindi cha usajili wa
dirisha dogo Januari mwaka 2013 akitokea Newcastle United, nyota huyo wa
kimataifa wa Senegal amefunga mabao 14 katika mechi 51 alizovaa jezi ya
Blues. Nyota huyo ameshindwa kutamba mbele ya Fernando Torres na Samuel
Eto’o na ujio wa mshambuliaji mpya Diego Costa kutoka Atleico Madrid
ndio uliomfugulia milango ya kutafuta klabu mpya huku meneja Jose
Mourinho akiwa tayari kupokea kitita cha paundi milioni 10 kwa mauzo
yake. Mwenyekiti wa Besiktas Fikret Orman amesema pamoja na kwamba
Chelsea waliweka dau la paundi milioni 10 lakini wamefanikiwa
kuwashawishi na kuteremsha kiwango hicho. Orman aliendelea kudai kuwa
wataufahamisha uma mara watakapomaliza hatua za mwisho za usajili huo.
No comments:
Post a Comment