Baada
ya kutatua tatizo la uandikishwaji wa wanafunzi wapya mashuleni na
vyuoni kila mwaka, karibu duniani kote,Hivi sasa kumeibuka tatizo jipya
la kufeli mitihani.Tatizo hili ambalo wengine kwa kuogopa neno matatizo
wamelibatiza jina changamoto, limekuwa kubwa karibu duniani kote.
Kwa ufupi karibu kila mahali duniani uandikishwaji (udahili) wa wanafunzi wapya umeongezeka.
Mfano
mzuri ni kwa Tanzania ambayo ni moja ya nchi ya mfano kusini mwa jangwa
la sahara. Ilitimiza dira ya maendeleo ya dunia ya elimu ya mwaka 2025
kwa kufikia uandikishaji wa 103% hapo mwaka 2012.Vile vile takwimu za
banki ya dunia zinaonyesha kuwa mpaka kufikia mwaka 2010 ilifikia 95.4%
ya uandikishaji wa wanafunzi kwa shule za msingi toka chini ya asilimia
60% mwaka 2000.
TAKWIMU KWA UFUPI
Mafanikio
hayo sio kwa Tanzania tu, bali zipo na nchi nyingine zilizofanya vizuri
katika uandikishaji wa watoto shule . Miongoni mwa nchi hizo ni
ARMENIA 114 mwaka 2009, AUSTRALIA 100% mwaka 2009,
BAHAMAS, THE 103% mwaka 2009 ambayo ilishuka 1% mwaka uliofuata,
BANGLADESH 105% mwaka 2009, GHANA 100% mwaka 2013,
GERMAN 100% mwaka 2009, CHINA 100% mwaka 2009,
GUYANA 108% mwaka 2009, UNITED STATES 100% mwaka 2009 na kushuka 2% mwaka 2012.
kwa nchi za afrika mashariki
KENYA 98% mwaka 2009 na hakuna takwimu kwa miaka iliyofuata,
UGANDA 102% mwaka 2011,
BURUNDI 99% mwaka 2012,
RWANDA 103% mwaka 2009 na kushuka 1% mwaka 2012.
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa bank ya dunia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule.
Kutokana
na kuongezeka kwa uandikishwaji wa watoto shule za msingi hata
sekondari na vyuo vimepata ongezeko kubwa la wanafunzi wapya kila
mwaka.Isingetosha kutazama takwimu kwakua sio mada yake.
TATIZO LA KUFELI MITIHANI.
Tatizo
hili limekuwa ni kubwa sana na kuwaathili wazazi ,walezi ,walimu
,serikali na hata wanafunzi wenyewe.Ukubwa wa tatizo umesababishwa na
wadau wenyewe wa elimu ikiwamo wanafunzi.Mbaya zaidi ni kwamba katika
kushughulikia hili tumejikita zaidi katika mambo ambayo yako nje ya
uwezo wetu na sio yaliyo ndani ya uwezo wetu.
Leo
ukimuuliza mtu kwa nini wanafunzi wanafeli mitihani? Atakujibu kirahisi
tu kuwa madawati hayatoshi.mwingine atakwambia walimu hawatoshi.
Ninachotaka
kusema ni kuwa hata kama kila mtu atakaa kwenye kiti chake darasani na
kupata mwalimu wa kumfundisha peke yake, kunauwezekano bado wa kupata
watu wanaofeli mitihani. Najua utashangaa kidogo kwa maelezo hayo yaliyo
kinyume kabisa na mawazo ya wengi.Ila utanielewa katika kipengele
kinachofuata.
KWA NINI WATU WANAFELI MTIHANI
Tatizo kuu la watu kufeli mtihani ni kutoelewa walichojifunza au kuelewa kwa kiasi kidogo sana.Kutoelewa kunatokana na sababu kadhaa ambazo zimeorodheshwa hapo chini tafadhali pitia kwa umakini.
1.UWEZO MDOGO WA KUELEWA HARAKA
Kila
mtu hapa duniani ana akili,tena akili za kutosha, isipokuwa kwa wale
wenye magonjwa yanayohusiana na akili.Kusema hivyo ni kwamba kila mtu anauwezo wa kufaulu mtihani, ilimradi tu kama alipata nafasi ya kujifunza.
Watu
wenye uwezo mdogo wa kuelewa haraka huwa wanafeli kutokana na kutopata
muda wa kutosha kueleweshwa.Kundi hili lina idadi kubwa sana ya watu
mashuleni kuliko wale wanaoelewa haraka.Kwa kawaida mwalimu hutumia
dakika zisizozidi 40 darasani akifundisha.Ni dhahili kuwa muda huu
hautoshi kufanya kila kitu kinachomwezesha mwanafunzi kubaki ameelewa
100%.Hivyo kundi la hawa wanafunzi wasioelewa haraka hubaki na pengo la kuelewa kila siku wanapotoka darasani.
Wakati
bado wanashughulikia pengo lao ili wafanane na wale wenzao walioelewa,
hujikuta wakikabiliwa na mitihani.Matokeo yake hujikuta wakijibu
mtihani ama kwa jinsi wanavyoelewa wao au kwa kubahatisha, hivyo kufeli
mtihani.
SULUHISHO.
Ni
vizuri kujikagua hasa kwa wale wanafunzi wakubwa, kama unatatizo la
kutoelewa haraka.Utafahamu kirahisi kama unatatizo hilo kwa kujipima na
wenzako ambao mnajifunza pamoja kwa kuona wakiwa wameelewa na wewe ukiwa
bado.Pia unaweza kujipima kwa kujiuliza maswali madogo madogo
yanayohusiana na ulichojifunza kuona kama unaweza kujijibu. Pia kwa wale
wenye watoto unaweza kumpima kwa kumlinganisha na watoto wengine au
kwa maswali madogo madogo.
Utatuzi sio kwenda ( kumpeleka mtoto) tuition, kwani hata huko unaweza kukumbana na tatizo lilelile.Cha kufanya ni kutumia muda mrefu zaidi kujifunza kitu kilekile hata kama ni kwa mwalimu yuleyule mpaka uelewe.Hapo
ndipo utakapoona unafaulu.kumbuka hata ulipoanza kujifunza kusema
ungali mdogo, ulikosea kila neno ,lakini kila siku ulirudia maneno
yaleyale mpaka sasa huhitaji hata kujikumbusha unapotaka kuyatumia.
2. ULEMAVU
Kama
mwanafunzi hajakaguliwa sawasawa kuhusiana na ulemavu na kuhudumiwa
kipekee ,kunauwezekano mkubwa wa kufeli mtihani.ulemavu ambao una
madhara makubwa sana katika ufaulu ni pamoja na ulemavu wa akili,uoni
hafifu na kutosikia vizuri.Kuna baadhi ya wanafunzi wenye uoni hafifu au
kutosikia vizuri wasiojulikana na walimu wao.Kwasababu ya kutojulikana
kwao hujikuta wakijifunza kwa mashaka tu mpaka mwalimu anamaliza
kufundisha darasani.Matokeo yake hujikuta wakiwa hawajaelewa mpaka
mitihani inapowakuta.
SULUHISHO
Ni
vema kujikagua au kumkagua mwanafunzi kama ana matatizo niliyokwisha
yataja.Endapo kama unamatatizo hayo au mojawapo basi ni vema kuhakiki
kuwa hayaathili kuelewa kwako.Kama yana athili basi tumia njia
inayokufanya uelewe na sio kubaki na deni la kutoelewa kila utokapo
darasani.
3.UWEZO MDOGO WA KUCHUKULIANA NA MAZINGIRA
Mwanafunzi
mwenye uwezo mdogo wa kuchukuliana na mazingira, anaweza kuelewa
taratibu au kutoelewa kabisa na kujikuta akifanya vibaya katika mitihani
yake.Hapa ndipo unapokuja ule usemi ninaoupenda sana usemao kile usichoweza kukizuia kiepuke.
Mazingira
yanaweza kumuathili mwanafunzi endapo kama hatoelewa nini cha kufanya
wakati yanapofikia hatua ya kuathili uelewa wake darasani.
Hapa
ndipo unapoweza kuona tofauti .Kwamba mwanafunzi anayeishi katika
mazingira magumu au kutoka familia yenye kipato kidogo na vyenzo chache
za kujifunzia anafaulu mtihani, lakini Yule mwenye kila kitu
anafeli.Yote inatokana na uwezo wa kifikra alionao mwanafunzi katika
kukabiliana na mazingira kama hayo.Uwezo huu huwa ni wa kibinafsi zaidi
na sio ule unaotokana na mafunzo maalumu.
Mazingira
yenye athali yanaweza kuwa uchumi duni,uhaba wa walimu au
wakufunzi,umbali wa shule au chuo,uwezo mdogo wa walimu au wakufunzi
kufundisha,nyenzo chache za kujifunzia au kufanya mazoezi
(practicals),changamoto za kirika (mapenzi,starehe).Hivi vyote ni
vikwazo katika kuelewa kwa mwanafunzi shuleni.
SULUHISHO
Kama
kunamazingira yeyote yanayokufanya au yanayomfanya mwanafunzi kushindwa
kuelewa darasani au kwingineko, jambo la kwanza ni kuyaepuka.Ikiwa ni
umbali tafuta kukaa karibu na shule/ chuo,kama ni uwezo duni wa walimu
au wakufunzi tafuta wakufunzi,kama ni nyenzo chache jifunze kutumia
zilizopo au zinazopatikana kwingineko.
Tafuta
na kuelewa kama udhaifu wa kuelewa kwako darasani unasababishwa na
mazingira uliyonayo. mazingira usiyoweza kuyakabili unachofanya ni
kuyaepuka .Kuepuka ni njia rahisi sana katika mapambano yeyote
yale.Nafikiri endapo kama utapewa miujiza ya kuweza kukwepa masumbwi
yoyote hapa duniani, basi ungelijitosa katika mashindano ya masumbwi ya
pesa nyingi kwa kutegemea uwezo wako wa kukwepa masumbwi.Ungefanya hivyo
kwa kuwa usingetegemea kupangua au kuhimili kipigo cha konde lolote
kutoka kwa mshindani wako kwa kuwa unauwezo wa ajabu wa kukwepa makonde.
Endapo
mazingira uliyonayo hayaepukiki basi njia ya pili ni kujenga nayo
urafiki ili uyatumie kwa manufaa yako.Anza kujenga ukakamavu wa kuishi
katika mazingira ambayo huyapendi ili yasiharibu uelewa wako darasani.
Sote tunafahamu kuwa gerezani ni mahala penye maisha magumu sana ,lakini mfungwa anaweza kuishi miaka 30 na zaidi.
Sote
tukisikia mlipuko wa bomu au risasi tunakimbia hovyo ,lakini askari
anaweza kukaa vitani na milipuko hiyo mpaka atakapopata amri ya mkuu
wake kuondoka ili asifukuzwe jeshini.
Sote
tunafahamu kuwa ni vigumu kwa binadamu yeyote kukaa macho usiku mzima
bila kulala, lakini leo tuna mamilioni ya watu duniani wanaokesha kwa
hiari yao viwandani ili mwisho wa mwezi waweze kujipatia kipato.
Kwasababu
hiyo hata wewe unaweza kujenga ukakamavu wa hiari kukabiliana na
mazingira uliyonayo ili yasipunguze uelewa wako darasani .Kwa kuzingatia
ushauri huu nina imani sasa hautafeli tena mtihani na utakuwa msaada
kwa wengine.
No comments:
Post a Comment