Breaking News
recent

ALAMA MPYA ZA UFAULU TANZANIA

Alama hizi ni kwa mujibu wa WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI.
Kutokana na taarifa ya serikali kupitia KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI ufuatao  ndiyo utaratibu mpya wa upangaji wa alama za ufaulu kwa kidato cha nne na sita.Utaratibu huu utatumika kwa mzunguko wa  miaka minne labda kama kutakuwa na ulazima wa kufanya mabadiliko kabla ya kipindi hicho.

Kuna miundo mikuu miwili ya upangaji wa matokeo .
      1.       Ule unaotumika katika kupanga matokeo shuleni.
      2.       Ule unaotumika katika kupanga matokeo baraza la mitihani.

Mgawanyo wa alama upo katika majedwari hapa chini kama yanavyojieleza na ufafanuzi wa ziada uko baada ya majedwari hayo.

JEDWARI NA .1. ALAMA ZA UFAULU ZILIZOZOELEKA MASHULENI MIAKA YOTE


1.

Kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade range) ulitumika,  ambapo wigo wa alama  ulibadilika badilika kulingana na ufaulu wa mwaka husika.mwaka 2012 serikali iliamua kutumia viwango vya alama mgando (fixed grades)kwa kidato cha nne na cha sita.mifano ya miundo iliyotumika ni kama unavyoweza kuona hapa chini.



JEDWARI NA . 2. ALAMA ZA UFAULU ZILIZOTUMIKA  MWAKA 2012 KIDATO CHA NNE.


2.

















JEDWARI NA .3. ALAMA ZA UFAULU ZILIZOTUMIKA MWAKA 2012 KIDATO CHA SITA.

3


Mifumo hii ya baraza haikuwa inafahamika sana hivyo kuleta manung’uniko katika secta ya elimu.hivyo serikali ikashirikisha wadau na kuja na mfumo huu hapa chini.


JEDWARI NA. 4. ALAMA MPYA ZA UFAULU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA 2014 KWA KIDATO CHA SITA.Huu ndiyo mfumo teule unaotumika sasa.


4
















JEDWARI NA  .5.  UFAFANUZI WA JEDWARI NA.4.   MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU.Huu ni muachano wa alama kutoka wigo hadi wigo.


5.


JEDWARI NA  .6.   UFAFANUZI WA ZIADA  JEDWARI NA.4.   MUUNDO WA MADARAJA.

6.


JEDWARI LA NYONGEZA NA.7.ALAMA ZA UFAULU KWA WATAHINIWA WA ELIMU YA MSINGI.Tazama hapa chini.


7.

Watahiniwa wa elimu ya msingi viwango vyao vya ufaulu vinapimwa kwa alama 250.Mfano halisi unaweza kuuona katika jedwari hilo hapo juu.


UFAFANUZI WA ZIADA KWA JEDWARI NA.1 ,2na3

Kabla ya mwaka 2012 yaani 1973 hadi 2011 Tanzania ilitumia viwango nyumbufu katika upangaji wa matokeo ya ufaulu  yaani (flexible Grade Range ).

Mwaka 2012 serikali iliamua kutumia viwango mgando yaani (fixed grades)katika kutunuku matokeo kwa wahitimu sekondari.Lengo la kufanya hivyo lilikua ni kuwaweka wazi wadau wa elimu kufahamu viwango vinavyotumika katika kupata matokeo ya ufaulu kwa wahitimu hao.

Pia wizara iliunda kamati maalumu ambayo ilipitia taarifa mbalimbali na kutoa mapendekezo ya  mfumo utakaofaa katika kuweka viwango vya ufaulu.mapendekezo hayo yalipelekwa kwa wadau mbalimbali ili watoe maoni kuhusu utaratibu mpya utakaoyumika katika kupata matokeo ya kidato cha nne na sita.

WADAU WALIOSHIRIKI KUTOA MAPENDEKEZO.

Jukwaa la Taasisi za Elimu ya juu,Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari Nchini (TAHOSSA) wakuu wa vyuo vya ualimu vya umma,Wamiliki na Wakuu wa Shule na Vyuo Visivyo vya Serikali (TAMONGSCO), wakaguzi wa shule kanda,Muungano wa Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO), viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,walimu, wanafunzi, wazazi, maafisa elimu Mkoa, Wilaya pamoja na maafisa taaluma wao,  wadau kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wanataaluma na Wanasiasa.

MATOKEO YA MAPENDEKEZO YA WADAU

      1.    Walipendekeza kuwa utaratibu wa mfumo nyumbufu (flexible grades) sio mzuri na badala yake utumike mgando (fixed grades).

      2.    Wadau pia walipendekeza kuwa muachano wa makundi ya alama uwe kwa kiwango cha alama kumi kumi.

      3.    Walipendekeza kuwa mfumo wa tahtimini ya matokeo endelevu au CA (Continuous Assessment) ujumuishwe katika kupata matokeo ya ujumla ya kuhitimu kidato cha nne na sita.mapendekezo hayo yalidai kuwa matokeo hayo endelevu ambayo ni yale anayoyapata muhitimu awapo shuleni yawe yanachangia kwa 40% na yale ya mtihani wa mwisho yachangie 60%.

Ikumbukwe kuwa katika sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 1995, matokeo endelevu kutoka shuleni yamepangwa kuchangia kwa 50%.Lakini tangu kuanza kutumika kwa sera hiyo utaratibu huo haujawahi kutumika.

(maana ya matokeo endelevu.ni matokeo anayoyapata mwanafunzi katika mitihani yake ya wakati wa maendeleo ya elimu yake kabla ya mtihani wa mwisho kuhitimu darasa la saba,kidato, cha nne au cha sita.)Matokeo haya katika sera ya elimu yamejumuhisha ufaulu kitaaluma,nidhamu,ushirikiano nk.

     4.    Walipendekeza kuwa ili kuimarisha uwezo wa kufikiri na kuandika kila mwanafunzi afanye project na matokeo yake yajumuhishwe kwenye matokeo ya mwisho.

     5.    Pia walipendekeza kumpa mwalimu fursa kwa kuchukua sehemu ya  matokeo ya muhula wa kwanza na wa mwisho wa kidato cha tatu katika kupata matokeo ya jumla.

     6.    Wengi walipendekeza kuwa muundo wa sasa wa madaraja uimarishwe na kuanzisha MUUNDO WA WASTANI WA UFAULU.(Grade Point Average au GPA)

     7.    Mwisho wadau walikubaliana kuujalibu utaratibu huu kama  mfumo halisi kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 na 2013 kwa kidato cha sita.Zoezi hili lilifanyika

MAAMUZI YA SERIKALI.

Serikali kupitia wizara ya elimu iliridhia sehemu kubwa ya maoni ya wadau kisha  kupendekeza na kutangaza viwango vipya vya ufaulu kwa mwaka 2013 kwa kidato cha nne na 2014 kwa kidato cha sita kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwari na.2 na 3.

UFAFANUZI WA JEDWARI NA 4..

     1.    Kwa wale wasiofahamu kila alama ina namba yake ya utambulisho inayotumika katika     kutoa points.kwa msaada zaidi tumia jedwari na 4.

      Mfano,chukulia mtahiniwa ana alama zifuatazo katika masomo yake. Uraia A,Jiografia B,historia A,Hisabati D,kiswahili A,Bailojia C,kiingereza C.kufahamu mtahiniwa huyu ana point ngapi, italazimu kufanya ifuatavyo.

      A+B+A+D+A+C+C=1+2+1+4+1+3+3=15
      kwa kuwa A=1,B=2,D=4 na C=3.Hivyo jumla ya points atakazokuwa nazo mtahiniwa huyu ni 15.Tukitaka kufahamu kuwa mtahiniwa huyu yuko katika daraja gani (division)Tunaweza kutumia jedwari la ufafanuzi na 6 hapo juu,ambapo atakuwa ndani ya point 17 ambazo ndiyo wigo wa daraja la kwanza.
  
      Kusema hivyo ni kwamba mtahiniwa ataingia kwenye daraja la kwanza moja kwa moja kulingana na point alizonazo.Unaweza kufanya hivyo kwa matokeo yeyote ukitumia majedwari hayohapo juu. 

     2.    CA( Continuous Assessment ) au tathmini ya matokeo endelevu ya sekondari yatatokana na mtihani

wa kidato cha pili (alama 15),

 Matokeo kidato cha tatu alama 10 kwa mihula yote miwili,

Mtihani wa mock alama 10,

Kazi mradi au projects alama 5.

     3.    KIDATO CHA SITA wao wataendelea na CA inayotumika sasa.

         WATAHINIWA BINAFSI AU PRIVATE CANDIDATES 

1.kwa wale wanaorudia mitihani yaani Reseaters CA zao zitatumika zile zilizotumika wakati wa mitihani yao ya awali.

2.Kwa wale waliopitia katika utaratibu wa QT(Qualifying Test) yaani mtihani wa maarifa Matokeo ya mtihani wa maarifa utatumika kama CA( Tathmini ya matokeo endelevu)kwa kuchangia 40% na matokeo ya mwisho yatachangia 60%

     5.    Muundo wa alama katika ufaulu (Grade Point Average) utaanza kutumika pale utakapokuwa tayari.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.