Jose Chameleon amewashtua mashabiki wake wa Uganda kwa kiingilio kikubwa sana kilichopangwa kwaajili ya kushuhudia show yake mwisho wa mwaka huu.
Hit maker wa ‘Tubonge’ Jose Chameleone anatarajia kufanya show yake iliyopewa jina la ‘One man, One show, One Stage” ambayo kiingilio chake kimepangwa kuwa shilingi milioni 1 ya Uganda (sawa na laki 6 ya Tanzania).
Inadaiwa kuwa kiingilio cha kawaida kwa show za kimataifa Uganda huwa ni kati ya Tsh 30,000 hadi 50,000.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Chameleon amesisitiza kuwa hawezi kushusha kiingilio hicho kwasababu wale wenye uwezo wa kulipa kiasi hicho ndio walengwa na ndio watakaokuja.
“I have never asked or even debated with any business institution how they determine their prices of their commodities.” Aliandika Chameleone.
“The One man, One night, One show, is NOT for anybody below affordance. Honestly it’s for the loyal Fans and The crowd that can’t come to the other usual venues. But am also very glad it’s the doubtful ones debating about it and doing me free advertisement unknowingly. The SHOW is ON !!! 19th December 2014″
Kama lilivyo jina la show yenyewe ‘mtu mmoja, usiku mmoja, show moja’, Chameleone mwenyewe ndio atatawala jukwaa mwanzo hadi mwisho wa show.
Show hiyo inatarajiwa kufanyika December 19 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment