Huku timu za Afrika zikilazimika
kusafirisha mamilioni ya dola za kimarekani hadi Brazil (Nigeria
Cameroon) ilikuzima migomo kabla ya mechi muhimu timu ya Ugiriki
ilifanya kinyume na hayo ilipokataa katakata kupokea malimbikizi ya
marupurupu yao kutoka kwa serikali .
Timu hiyo iliyoondolewa na Costa Rica katika
mkondo wa pili ilimwandikia waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras barua
ikimtaka atumie fedha hizo kujenga uwanja mpya wa kandanda utakaotumika
kutambua na kukuza vizazi vipya vya kandanda.Bwana Samaras aliahidi kutekeleza ombi la wachezaji wake alipozungumza kwa njia ya simu na maafisa wa shirikisho la soka la Ugiriki.
No comments:
Post a Comment