1. Bado uko hai na una afya njema.
2. Unaweza kuona kuchomoza na kuzama kwa jua.
3. Hukulala bila kula usiku wa kuamkia leo.
4. Umeamka leo asubuhi ndani ya nyumba yenye paa.
5. Baada ya kuoga una uwezo wa kuchagua uvae nguo gani kati ya nyingi ulizo nazo.
6. Hujapatwa na wasiwasi kwamba dakika yoyote leo hii unaweza kupoteza maisha.
7. Umepitia mambo makubwa, ya kuogopesha na mengine ya kukatisha tamaa kwenye maisha lakini umeyashinda na leo bado upo.
8. Huwa unatumia baadhi ya muda wako kuwaza kuhusu kazi, familia, mipango yako ya miaka miwili au mitatu ijayo - hii inamaanisha kwamba bado una imani utaendelea kuwa hai, una kiu ya kuwa bora zaidi kesho na una uhuru wa kupanga mambo yako.
9. Una familia na marafiki ambao mara kwa mara wanatumia kiasi cha muda wao kukukumbuka.
10. Una baadhi ya watu unaweza kuzungumza nao mkafurahi kuhusu maisha ya miaka iliyopita.
11. Unaweza kupata maji ya kunywa safi na salama.
12. Ukiugua una uhakika wa kupata tiba.
13. Unaweza kusoma na kuandika.
Ukweli ni kwamba kama una hayo maisha yako ni bora kuliko watu wengi sana katika dunia tunayoishi. Shukuru kwa yale uliyojaaliwa.
No comments:
Post a Comment