Yusta Lucas akionyesha makovu yake ya mgongoni ambayo aliyapata kwa kung'atwa na kuchomwa na pasi na mwajili wake. Picha na Esther Kabakay
Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.
Binti huyo, mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika
Kijiji cha Kampala amedai kuwa amekuwa akiteswa na kufungiwa ndani ya
nyumba na tajiri yake, Amina Maige wa Mwananyamala, Kwa Manjunju katika
kipindi chote hicho. Amina anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha
Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba OB/RB/9967/2014.
Akisimulia masahibu yaliyompata akiwa katika Wodi
Namba Tatu ya hospitali hiyo, Yusta alisema: “Nililetwa Dar es Salaam
mwaka 2010 kufanya kazi za nyumbani baada ya bosi wangu (Amina) ambaye
ni binamu yangu kuzungumza na mama yangu na kuniomba nije kumsaidia kazi
ndogondogo.”
Alisema aliishi vizuri na mwajiri wake huyo,
lakini mwaka 2012 ndipo mambo yalipoanza kubadilika akidai kuwa Amina
alianza kumwadhibu kwa kumng’ata na kumchoma kwa pasi kila alipomtuhumu
kutokufanya kazi zake vizuri.
“Alikuwa akinichapa na kuning’ata sehemu
mbalimbali wakati mwingine usoni, pia kunichoma kwa pasi yenye moto kila
aliponituhumu kutokufagia au kupiga deki vizuri.”
Hakuwahi kupelekwa hospitali
Alisema licha ya kupata vidonda kutokana na adhabu
hizo, mwajiri wake huyo hakuwahi kumpeleka hospitali na pale alipoona
hali ni mbaya alimnunulia dawa... “Tunaishi wawili tu baada ya kuondoka
mumewe na mtoto wake kumpeleka shule ya bweni... niliugulia hadi
nikapona bila mtu mwingine kufahamu.”
“Akienda kazini anafunga geti na kunikataza
kufungua hata kama mtu atagonga… sokoni nilikuwa naenda siku ambazo yeye
yupo tu na huwa akiniamrisha niende haraka na kurudi pasipo kuzungumza
na mtu yeyote.”
Alisema mwajiri wake huyo alikuwa akituma pesa za
mshahara wake kwa mama yake akisema ndiye anayepaswa kulipwa, jambo
ambalo anadhani limemfanya mama yake kuhisi mwanaye yuko katika mikono
salama... “Kila alipotuma alipiga simu na kunipa niongee na mama
kuhakikisha kama zimefika huku akinisimamia na baada ya hapo anachukua
simu.”
Ataka kurudi kwao
Binti huyo ambaye sehemu
kubwa ya mwili wake ina alama za kung’atwa meno na majeraha ya kuchomwa
na pasi, alisema: “Ninaomba mtu yeyote mwenye hela, nataka nikitoka
hapa hospitali nirudi Tabora kwa mama. Nina shaka na maisha yangu hapa
kwa huyu mama… sitaki tena kubaki Dar es Salaam kutokana na mateso
ninayoyapataSOURCE: Nice MediaWorks
No comments:
Post a Comment