HIVI NDIVYO MWANAFUNZI ANAWEZA KUJIONGEZEA UELEWA...
Tatizo la wanafunzi wengi siku hizi wamekuwana mtindo unaoitwa ‘copy and paste ’ yaani
anachofundishwa ndicho wanachokishika na wakati mwingine kukiandika, jambo ambalo
huchagia kuwafanya washindwe kuwa naufahamu wa kutosha juu ya mambowanayoyasoma.
Katika hali ya kawaida kazi kubwa ya mwalimu ni kumpa mwanafunzi moja kati ya mambo
manne yanayokamilisha pembe nne za kuta ya ufahamu. Hii ina maana kwamba mwanafunzi anayepewa
moja na mwalimu hawezi kuwa imara kama yeye mwenyewe hakujenga kuta zake tatu za kujielewesha.
Haifai kuwa mwanafunzi mwenye mfano wa kasuku, kuiga kilichofanywa na mwingine.
Lazima katika kila unachofundishwa , uhakikishe kuwa unapata muda wa
kukichambua kwa kina na kuzidi kujielimisha zaidi ya pale alipoishia mwalimu .
Njia pekee ya kufikia kiwango cha juu cha uelewa ni pamoja na kupata muda wa
kuchambua na kutafiti kile ulichofundishwa na kupata muda wa kuwashirikisha wengine kile
unachokijua zaidi ya ulichofundishwa darasani . Mwanafunzi ambaye atakuwa na tabia ya
kuwaeleza au kuwafundisha wenzake anachokijua zaidi kuhusu jambo fulani ndiyo
atakuwa anajijengea uwezo wa kufahamu zaidi na kuimarisha kumbukumbu za kile alichofundishwa.
Kilio cha wanafunzi wengi siku hizi ni usahaulifu. Ukichunguza kwa makini utagundua
kuwa, usahaulifu huo unatokana na tabia ya kukariri kama kasuku na kutokuwa na muda
wa kushirikiana na wenzake katika mijadala ya kujielimisha.
Nashauri kila unachojifunza pata muda wa kukichambua kwa kina na pendelea zaidi
kuwafundisha na wengine juu ya kile ulichopata katika kujielimisha kwako.
Upana wa elimu haupatikani darasani bali kwenye upembuzi yakinifu juu ya masuala
mazima ya dunia , huku njia pekee ikiwa ni kusoma vitabu na machapisho mbalimbali na
ushiriki wa moja kwa moja katika uvumbuzi wa vitu vipya ambavyo wakati mwingine
havijaandikwa wala kusimuliwa . Shida kubwa ya wanafunzi wa leo kama nilivyosema ni kukariri jambo linalowakosesha ufahamu. Kwa mfano , mtu anaweza kufundishwa uandishi wa habari na akachagua
michezo kuwa ni sehemu ya uandishi wake lakini ukimuuliza mtu huyo huyo anawafahamu
wachezaji wa Yanga na Simba ? Jibu litakuwa hapana, sasa mwandishi wa aina hii atafaa nini
kwenye soko la habari? Kujielimisha ni bora zaidi ya kufundishwa .
Kasoro hii ipo kwenye taaluma nyingi, wanafunzi wanahitimu lakini wanakosa uwezo
wa kutumikia elimu zao kwa sababu maisha si kitu cha kukariri, ni sanaa ya kujifunza , tena kila siku.
Mtu anaweza kuwa na digrii ya karatasi lakini kichwani akawa ni ufahamu wa darasa la saba,
haya ndiyo yanayojitokeza kwa wanafunzi wengi siku hizi ambapo tatizo pekee la
wasomo wetu wamegeuka watu wa kunakiri bila kuchunguza kwa kutumia akili zao , jambo
ambalo ni la hatari.
No comments:
Post a Comment