Breaking News
recent

MILLEN MAGESE AIDONDOKEA SERIKALI NA KUOMBA SUPPORT KWA WANANCHI..


Alidondosha chozi

Huyu dada alikuja kutokea Mwanza kumwimbia Millen shahiri


Alimgusa sana Millen hadi akalia

Akaanza kutoa somo kwa wanawake waliojitokeza

Miss Tanzania 2010 Geneviv Mpangala aliwakuwapo kumpa sapoti

Dokta Belinda Ballandya

Mratibu wa Miss Temeke Benny Kisaka akiwa na mamiss wake


Dokta Belinda Ballandya na Dokta Fadhlun hao waliokaa kushoto wametokea Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili 

Group picture  

Team nzima ilikuwapo


Geneviv akashow some love


Millen na wadau huyo  janaa anaitwa Evance nyuma yake ni Lucy Ngongoseke wa Tabasamu Pr
Na Mwandishi Wetu
 MWANAMITINDO wa kimataifa wa hapa nchini na Miss Tanzania 2001 anaefanya kazi yake hiyo nchini Marekani Millen Magese ameiomba serikali kumpatia eneo ambalo atalitumia kujenga hospitali maalum ya kushugulikia afya ya wanawake.

Millen alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na watu mbalimbali waliohudhuria semina ya bure kuhusiana na hali ya Endometriosis inayowakabili wanawake wengi hapa nchini na Afrika kwa ujumla.

Millen anakabiliwa na tatizo hilo la Endometriosis ambalo ni hali ya mwanamke kushindwa kupata siku zake za mwezi katika hali ya kawaida na yenye kuleta madhara kwa afya yake hususan kwenye uzazi.

Millen alisema kuwa akiwa kama mwanamke maarufu na mwenye ushawishi katika jamii yake ameamua kutoa elimu ya tatizo hilo ili kusaidia kuongeza uwelewa wa suala hilo ili kuwasaidia wanawake wengine.

Alisema kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiana na afya hivyo linahitaji msaada wa ukaribu zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya kusaidia wasichana na wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya pia.

Alisema kuwa mwanamke anaekabiliwa na tatizo kama hilo anafikia wakati anakuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji na lakini kutokana na ugeni wa tatizo husika kwa hapa nchini hakuna vifaa vya kutambua na kufanyia upasuaji huo. Ambapo mpaka sasa ni KCMC pekee ndio wana kifaa cha kuweza kutambua tatizo hilo.

Alisema kuwa ameshaanza kupata misaada kutoka kwa watu mbalimbali wa Marekani kama vile taasisi ya Swan Development LLC, Texas ambao wameahidi kumpatia mashine za za kutambua tatizo na upasuaji pamoja na dawa, ambapo angependa ziwekwe hospital ya Dar es salaam kulingana na mapendekezo ya wadau ingawa lengo lake la muda mrefu ni kufungua hospital itakayojihusisha na magonjwa ya wanawake na ndio maana anaomba msaada wa serikali na wananchi kwa ujumla ili kufanikisha lengo hilo.

"Ningependa kama kufungua hiyo hospitali basi iwe ni Dodoma au Bagamoyo kwa kuwa ni rahisi zaidi kwa Dodoma watu mbalimbali kufika na kwa Bagamoyo inakuwa ni rahisi pia kuzifikisha mashine kutoka Bandarini"alisema Millen.

Aliongeza kuwa kwa kuwa tatizo hilo linakuja kutokana na kushindwa kulishughulikia mapema hasa wakati msichana anapokuwa amevunja ungo na kuanza siku zake za hezi akiwa na maumivu makali.

Aliwataka watoto kuwaambia wazazi pindi wanapokuwa wakipatwa na maumivu makali yaliyopitiliza wakati wakiwa kwenye siku zao za hezi na pia wazazi kujadiliana na watoto wao punde hali hiyo inapotokea na kuwawahisha hospital ili wapatiwe huduma sahihi.

Katika tukio hilo la jana Millen aliambatana na madaktari bingwa wa wanawake wawili ambao ni daktari Fadhlun M. Alwy na daktari Belinda Ballandya wote kutoka chuo kikuu cha Afya Muhimbili ambao walitoa elimu ihusianayo na tatizo hilo na Endometriosis.

Watu wengi walijitokeza kupata somo hilo na kuzungumzia suala hilo wakiwemo, wanawake, wananume na watoto.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.