KUNA uwezekano Mkubwa kabisa ukajiuliza maswali
mengi kuhusu Kurudi kwa mahusiano ya Chris Brown na KarreucheTran, baada ya
Breezy kutoka Jela, huku awali ikibainika kuwa alikuwa amepigana Chini na
mamito huyo, lakini Hivi Ndivyo inavyoanza kuhisiwa.
Siku ya jana , TTM tulipata Mtonyo na Baadhi ya
Picha ambazo zilimuonesha Chris Brown akiingia na Kutoka kunako Night Club
Moja, akiwa na Girlfriend wake Huyo, Karreuche, kwa ajili ya Bata za hapa na
Pale, lakini baada ya kitengo CHIMBUA CHIMBUA kuzama Kiundani zaidi, kuna hili
ambalo limesomeka.
Karreuche Tran hakuwa karibu sana na Chris Brown
ndani ya Night Club Hiyo tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa, zaidi ya Kustick na
Bibie wa YMCMB, CHRISTINA MILLIAN.
Tofauti na kuwa na Christina, Karreuche alikuwa
busy akipiga mtungi wake kawaida, pamoja na Kucheza Mikwaju kadhaa ambayo
ilionekana kumuingia, huku Breezy akiwa haishi kumkata Jicho mara kadhaa, hali
ambayo iliashiria kuwa huendawawili hao, hawakuwa Vizuri.
Aidha katika Hali Nyingine ambayo ilizua maswali
kwa Wengi, Chris Brown alionekana kutokufurahia kabisa Usiku huo ndani ya Club
hiyo inayofahamika kwa Jina la SOCIALITE CLUB, inayosifika kwa Kuwahusisha
Wapenzi wa Jinsia Moja, huku karreuche akiwa katika Mood Nzuri.
Pia Bibie huyo alionekana kuwa Bize zaidi na
Simu kulikokuwa Busy na Chris Brown, lakini baadaye inasemekana kuwa baada ya
kutoka Nje kupokea Simu aliyopigiwa na Mtu ambaye hakufahamika mara
Moja,aliizima kabisa.
Chris Brown na Karreuche, wamekuwa wakipigana
Chini na Kurudiana tangia wameanzisha Mahusiano yao mwaka 2010, ikiwa ni baada
ya Breezy kuachana na Rihanna mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment