Breaking News
recent

KAMPENI YA "UKATILI SASA BASI" MBIONI KUZINDULIWA...


Kutokana na matukio ya ukatili yanayoendelea kulikabili taifa kwa sasa,baadhi ya watu wenye lengo na mitazamo chanya wameamua kujikusanya pamoja na kuunda kundi linalokwenda kwa jina la U7(usaba).Kundi hilo ambalo chimbuko lake ni watu mbali mbali walio kwenye mitandao ya kijamii wameamua kujikusanya pamoja na kuanzisha harakati zinazokwenda kwa jina la UKATILI SASA BASI ambazo zina nia na lengo la kupinga ukatili  nchini.
    Akiongea na mtandao huu Mwenyekiti wa muda wa kundi hilo Bw.Gwamaka Jongo amesema kundi hilo lenye maskani yake facebook kupitia jina la kundi UKATILI SASA BASI limeanzishwa ikiwa ni kampeni ya kumaliza kabisa ukatili unaoshika kasi kwa sasa hapa nchini hususani matukio kama lile la mtoto Nasra aliyefungiwa ndani ya boksi nk, "Tumeamua kulivalia njuga swala hili kutokana na matukio makubwa na yanayochafua jina la nchi yetu ambayo kimsingi sisi kama jamii tunauwezo kabisa wa kuyakomesha kwani hawa watendaji wa  haya matukio tunao humuhumu ndani ya jamii na wengine ni ndugu na jirani zetu""
     Aidha bw.Jongo aliuambia mtandao huu kuwa lengo kuu la U7 ni kuona kunakuwa na jamii yenye upendo na amani pasipo ukatili wala manyanyaso, "Lengo letu kubwa nikuona amani inatawala jaman,pia tunataka kuona nchi yenye upendo na isiyo na watu wanaonyanyasika kama tulivoona kwa baadhi ya watu ambao wengine wamepoteza maisha .Tunaomba sana tena sana jamii iungane nasi kwa dhati kabisa na tushirikiane kuwafichua hawa wanaotenda huu ukatili na tuwaripoti ili sheria zichukue mkondo wake.Ni imani yetu kwa pamoja tukipata ushirikiano kutoka kwa jamii na kila mmoja wetu kwa nafasi yake akajitoa na kuwaripot hawa watenda ukatili basi tutafanikiwa na taifa litakuwa na amani,upendo na furaha".
    Kuhusu  kampeni hii ya UKATILI SASA BASI Bw.Jongo amesema "Tunatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa kundi hili pamoja na harakati zake,ambapo tunatarajia kufanyia mkoani Morogoro ambapo ndipo mtoto Nasra alipofanyiwa ukatili uliompelekea umauti,ni imani yetu mapema iwezekanavyo tutafanya hivo na tutaanza rasmi harakati za kuhamasisha watu wote kuungana nasi.Pia tunaomba sana kila mtu mwenye malengo mema na nchi hii aungane nasi sasa,na kwa makampuni yote yenye malengo mema pia yatuunge mkono katika harakati hizi ili tuwepo nchi nzima na tufanikiwe kuutokomeza ukatili ,bila kusahau tunaiomba serikali kupitia jeshi la polisi na watu wa ustawi wa jamii kuunga mkono harakati zetu na kupokea taarifa za ukatili popote tanzania".
    Kwa yoyote atakayeguswa na kutaka kuungana na harakati hizi za  kupinga ukatili Tanzania basi ajoin kwenye group ya facebook yenye jina UKATILI SASA BASI au 0717520009 kwa mawasiliano zaidi.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.