KOCHA `mbwatukaji` Jose Mourinho amekiri kuwa Chelsea inavutiwa kumsajili Cesc Fabregas kutoka klabu ya FC Barcelona, huku mchezaji mwenzake wa Hispania Gerard Pique amesema dili hilo limekamilika kwa paundi milioni 26.8
Kocha
huyo amesema kuwa ni wazi Fabregas anataka kurudi ligi kuu ikiwa ni
miaka mitatu imepita tangu aondoke Asernal, hivyo anafuatilia kwa makini
ili kumsajili baada ya kombe la dunia.
Wakati
huo huo Chelsea wako tayari kumpa ofa ya mshahara wa paundi milioni
laki mbili kwa wiki winga wao hatari, Eden Hazard ili kuwaziba mdomo
Paris Saint-Germain wanaoiwinda saini yake.
“Kuna
mchakato huko anakotaka kuondoka, anataka kuja England kwasababu ni
taifa analopenda kucheza. Tunavutiwa kufuatilia hali halisi”.
Wakati
huo huo, Pique kwa upande wake anasema dili hilo limekalimika. Beki
huyo wa Hispania alinaswa na Kamera mjini Washington akimwambia kocha wa
Hispania , Vicente del Bosque kuwa Fabregas ataondoka Barcelona kwa
dau la paundi milioni 26.8 baada ya klabu hiyo kumalizia msimu bila
kikombe.
Gerard Pique alinaswa na kamera akimwambia kocha wa Hispani Vicente del Bosque kuhusu kuondoka kwa Fabregas.
No comments:
Post a Comment