Mkurugenzi wa kituo cha habari za serikali Dennis Katungi amenukuliwa akisema kuwa “Rais ana tabia zake wengi mnajua, huwa anatafakari na wanajua lakini bado wameonyesha picha hizo na kusema alikuwa amesinzia.”
Msemaji wa serikali Ofwono Opondo amethibitisha kuwa NTV Uganda itachukuliwa hatua za kinidhamu ambapo wameifungia kuripoti habari zozote zinazomhusu rais wakati bado serikali ikiangalia uhusiano wake na chombo hicho.
Ameituhumu NTV kwa kukosa utaalamu wa uandishi na kuegemea upande mmoja lakini hata hivyo hatua hiyo si ya kudumu ni ya muda tu kuwafanya wafikirie upya.
No comments:
Post a Comment