Majeruhi: Yaya Toure, akiwa mazoezini jumatatu, anaendelea kuimarika kwa kasi kuelekea mchezo wa ufunguz
KIUNGO
wa Ivory Coast,Yaya Toure anaendelea kuimarika kwa kasi kuelekea katika
mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia dhidi ya Japan jumamosi, amesema
kocha Sabri Lamouchi.
Toure ameshindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake tangu alipofanyiwa upasuaji mwezi uliopita.
Lamouchi
amesema timu ya madaktari wa Ivory Coast inajitahidi sana kuhakikisha
mchezaji huyo bora wa mwaka wa Afrika anacheza wakati nchi yake
itakapoanza mchezo wa ufungizi wa kundi C dhidi ya Japan mjini Recife.
‘Tunafanya kila linalowezekana ili acheze” kocha aliwaambia waandishi wa habari.
Toure
alipata majeruhi katikati ya mwezi aprili mwaka huu, lakini alirudi
uwanjani kuisaidia Manchester City kutwaa ubingwa wa pili katika misimu
mitatu.
Halafu akaenda Qatar kwa ajili ya matibabu na baadaye alijiunga na kikosi cha Ivory Coast kwenye kambi ya mazoezi huko America.
Toure hakucheza mechi mbili za kupasha pasha dhidi ya Bosnia na El Salvador.
SOURCE: SHAFII DAUDA
No comments:
Post a Comment