Mchekeshaji
wa muda mrefu Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ametoa kali ya
mwaka baada ya kusema kuwa maisha yake ni komedi tosha
kutokana na kumvunja mtu mbavu bila kujali yuko mahala gani….
Akizungumza
na mwandishi wetu, Mzee Majuto alisema yeye hutoa shoo muda
wowote bure bila kujali yuko katika wakati gani kwani maisha
yake ni komedi tupu…
“Maisha
yangu ni komedi tosha,siwezi kuacha kuchekesha.Wakati mwingine
si kwa kupenda bali huwa najikuta tu nimefanya hivyo , inabidi
watu wanizoee tu….
“Huwa
sina nia ya moja kwa moja kuchekesha watu, lakini kumbe kauli
zangu huwavunja mbavu.Sijisikii vibaya kwa hilo, najivunia
kuendelea kuwa msanii ninayekubalika hadi umri huu,” alisema mzee Majuto
No comments:
Post a Comment