Kwenye rada: Bastian Schweinsteiger anawindwa na Manchester United majira ya kiangazi mwaka huu. KLABU ya Manchester United inamuwinda zaidi Bastian Schweinsteiger katia usajili wa majira ya kiangazi mwaka huu. Mtandao huu kupitia mtandao rafiki wa Sportsmail iliweka wazi mwezi uliopita kuwa Man United wanavutiwa na nyota huyo mwenye miaka 29.
Schweinsteiger kwa upande wake tayari ameshaonesha nia ya kujiunga na bosi wake wa zamani Louis van Gaal katika dimba la Old Trafford.
Van Gaal ndiye aliyembadilisha Schweinsteiger kutoka nafasi ya winga na kuwa kiungo wa ulinzi na amecheza kwa mafanikio katika nafasi hiyo.
Mholanzi Van Gaal ambaye kwasasa anaiongoza Uholanzi katika fainali za kombe la dunia anamuona kiungo huyo kama mchezaji muhimu kwa Man united msimu ujao.

Louis van Gaal alifanya kazi kwa mafanikio na Schweinsteiger akiwa Bayern Munich
Schweinsteiger ni sehemu ya kikosi cha Ujerumani katika fainali za kombe la dunia, lakini nafasi yake ni wasiwasi.
Schweinsteiger alishinda kombe la Bundesliga na German Cup chini ya Van Gaal akiwa Bayern Munich.
No comments:
Post a Comment