WANASEMAGA, Ukiwa na Mkwanja, basi unaweza fanya
chochote ambacho unajiskia kufanya, na hicho Ndicho Rapper Kanye West
amthibitisha, TTM tuna Mtonyo Kamili.
Kuna uwezekano Mkubwa kabisa kuwa katika Jengo
kubwa la Kifahari ambalo linajengwa Kwa ajili ya Familia ya Kanye West huko, LOS
ANGELS, Nchini Marekani, itapatikana Hospitali Ndogo ambayo itakuwa ni Maalum
kwa ajili ya Familia Yake.
Kwa Mujibu wa Kitengo aminifu cha Chimbua
Chimbua kutoka TTM, Kanye ambaye hivi sasa ana umri wa Miaka 37, anatarajia
kutumia EURO MILIONI 3 kwa ajili ya kujenga Hospital Hiyo ndogo ambayo ni
mahsusi kabisa kwa ajili ya Afya yake, Mke wake Kim kardashian, pamoja na Mtoto
wao North West Mwenye Umri wa Mwaka mmoja hivi sasa.
Aidha katika Hospitali ndogo hiyo ya Ndani,
itajumuisha Vitu vifaa kama Vile Mashine ya X-RAY, CT Scanner, ULTRA SOUND
MACHINE, na Vifaa vingine kwaajili ya Kuchukua na Kupima Damu.
Tofauti na Vifaa hivyo, Pia Kanye anatarajia
Kuwaajili Madaktari na Wauguzi ambao watakuwa wakifuatilia afya za Familia Hiyo
mara kwa mara, pamoja na Timu maalum ya kumtizama na kuwa makini na Mtoto wake
North West..
Katika hali Nyingine, Kim Kardashian anaamini
kuwa Mme wake Huyo Kanye, anaenda Mbali sana katika maamuzi hasa ya Kujenga
Hospitali hiyo katika jumba lao, kwani ni kitu ambacho hakina ulazima sana kuwa
nacho, lakini hakuna ambacho anaweza fanya ili kumzuia Yeezy.
Moja kati ya watu maarufu ambao wamewahi kujenga
Hospital Ndogo katika Nyumba zao ni pamoja na Muimbaji mkongwe wa POP, MADONNA.
Kanye West na Familia yake hivi sasa wanaishi katika Nyumba ya Mama Mkwe Wake, KRIS JENNERS, wakati wakisubiri kumalizika kwa Ukarabati wa Jumba lao hilo huko LA, na wanatarajia kuhamia katika jumba hilo baada ya kila kitu kuwa sawa
No comments:
Post a Comment