Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama
yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye
familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara nyingi wasanii
wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia
walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha
nana elimu yake kuishia A’level , Hawa wengine walikua wapo shule
wakisoma na kuishi vizuri. Vibe Tanzania inawaorodhesha baadhi ya watoto
wakishua ambao kwasasa ni celebrities…
Vanessa Mdee
Vanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee
au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa
na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni mtu mzito
kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa na umri mdogo Vanessa
aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya
New York , Paris , Nairobi na Arusha.
Nisher
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza
huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher
amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake
aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni
15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.
Jokate Mwengelo
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku
baba yake akifanya kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa washington
DC nchini Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko.
Alipomaliza high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss
Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.
Wema Sepetu
Wema Sepetu ni msichana anayetoka
kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya
wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema sepetu
alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar
es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku akisoma elimu yake ya
primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo
jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya
biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.
Lucci
Jina lake halisi anaitwa Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci
ambaye ni producer maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30 September
mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na
akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci naye kama jokate
amekulia Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa
Tanzania.
SOURCE : MDADISI WA MAMBO BLOG
Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment