Mussa Leonard Mdede Aliyesimama |
Rais wa chuo kikuu Bugando Mussa Leonard Mdede amesema alitekwa na watu
asiowafahamu siku ya jumatano ya tarehe 18/6/2014 majira ya jioni
wakati akiwa katika maandalizi ya mwishomwisho kurudisha form ya kuwania
urais wa chuo hicho kwa muhula mwingine,akiongea na mwandishi wa habari
hii jana nje kidogo ya jijini la Mwanza ,bwana Mdede anasema licha ya
kwamba hakumbuki lolote lile lililotokea,lakini anashawishika kuamini
alitekwa na watu asiowafahamu kutokana na mazingira halisi anayoendelea
kusimuliwa na watu wake wa karibu juu ya sakata hilo.
Itakumbukwa
kuwa taarifa za kutoweka kwa Mdede katika mazingira ya kutatanisha
zilianza kusambaa tarehe 18 mwezi huu,ambapo taarifa za awali zilidai
kwamba,Mdede alitoweka majira ya jioni wakati akijiandaa kurudisha form
ya kuomba kuteuliwa kuwania urais wa chuo hicho kwa muhula
mwingine,Mdede ambaye pia ni rais wa TAHILISO hakupatikana kuanzia
tarehe hiyo mpaka jana usiku licha ya juhudi mbalimbali za kumtafuta
kufanyika ikiwemo kulihusisha jeshi la polisi mkoa wa Mwanza,taarifa za
kupatikana kwake zilianza kusambaa jana majira ya usiku,huku ikidaiwa
aliokotwa na watu wasiofahamika eneo la Usagala lililopo jijini hapa.
Akiongea
na mwandishi wa habari hii aliyemtembelea sehemu hiyo ambayo kwa sababu
za kiusalama blog hii ya http://nicholauskilunga.blogspot.com/,
haitafichua
mahala hapo kwa kupataja,rais huyo alisema"kwanza ninamshukuru Mungu
kwa kuwa watekaji wangu hawajanidhuru roho,lakini kimsingi sikumbuki
lolote kuhusu utekwaji wangu ama kutoweka kwangu,nayoyakumbuka ni ya
jumatatu ile,ila kwamba nilikuwa wapi,na kina nani ama nilifikaje hapa
nyumbani sijui kabisa,kila nikijaribu kuvuta kumbukumbu
zinakataa"alisema Mdede,hata aliendelea kusema hata hakumbuki kama
alikuwa katika mchakato wa kugombea urais wa chuo huku akijiuliza watu
waliokuwa wamemteka wamemfanyia kitu gani kilichomwondolea kumbukumbu
kiasi hicho,kwani hana jeraha sehemu yeyote zaidi ya kusikia maumivu
sehemu ya kichwa na maumivu ya mgongo,huku akisema anashindwa
kumuhusisha mtu yeyote katika sakata hilo kutokana na kwamba katika
siasa na uongozi ana maadui wengi ambao wanaweza kuwa wametokea katika
kundi lolote kati ya hayo,kitu ambacho kinampa ugumu kuunganisha na
kujua nani ama kinanani wamehusika kumteka.
Nae waziri mkuu wa
chuo hicho Benjamini Thomas alisema ,anamshukuru Mungu rafiki yake na
kiongozi wake amepatikana kwani alikuwa hana amani hasa kwa kuzingatia
hali ya usalama hapa nchini si nzuri na matukio ya utekaji na kujeruhi
yakiongezeka ,huku mamlaka husika zikishindwa kutoa majibu mujarabu,huku
akiishukuru tume ya uchaguzi ya chuo hicho na uongozi wa juu kwa ujumla
kwa busara yao ya kusitisha mchakato wa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike
tarehe 29 mwezi huu.
Bwna Mdede alipoulizwa na mwandishi wa blog
hii kama anatarajia kuendelea na harakati zake kisiasa na hasa kuhusu
kuendelea na harakati zake za kugombea urais wa chuo chake cha
Bugando,bwana Mdede alisema kwa sasa hawezi zungumzia mambo hayo,bali
amejikita katika kuiangalia afya yake na kuiimarisha ili itengamae,na
kwamba siasa zipo tu na zitaendelea kuwepo,lakini hajakatishwa tamaa
hata kidogo,huku akiishukuru familia yake,viongozi wake wa Bugando,SAUT
na vyuo vingine kwa kuchagiza utafutwaji wake.
Mdede alisema
anahisi sababu kubwa ya maswahibu yanayompata ni kutokana na misimamo
yake,na ndo anahisi imemponza,hasa katika kusimamia kile anachokiamini
akiwa kama mwenyekiti wa TAHILISO na rais wa Bugando,huku kaka yake
aliyeomba hifadhi ya jina lake anasema yeye anawatilia shaka watu
walimleta mdogo wake nyumbani kwake kwani maelezo yao yanatia
shaka,anasema "watu wale wanadai walimuokota mdogo wangu katika eneo la
Usagala akiwa hajielewi na wakamchukua na kumpeleka Igoma,sasa hapa
swali la kujiuliza ni kwanini waamue kwenda nae kwao Igoma na si kituo
cha polisi ama hata kwa uongozi wa serikali ya mtaa?"alitoa wito kwa
jeshi la polisi kufanya uchunguzi zaidi na kwamba wanaweza hata kubuni
picha za watu wale waliompeleka mdogo wake nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment