NYOTA wa Ufaransa, Franck Ribery atakosa fainali za kombe la dunia baada ya kushindwa kupona majeruhi yake ya mgongo.
Ribery pamoja na kiungo wa Lyon Clement Grenier wameondolewa rasmi katika kikosi cha Ufaransa kutokana na majeruhi.
Winga
wa Bayern Munich, Ribery amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mgongo na
amekuwa akifanya mazoezi peke yake mpaka leo hii alipojiunga na wenzake
mazoezini.
Ribery
aliyeichezea Ufaransa mechi 80 ni mchezaji muhimu kwa Deschamps na
kumkosa katika fainali za kombe la dunia ni pengo kubwa mno.
Ribery ameshindwa kupona kwa wakati.
Fursa: Mchezaji wa Southampton, Morgan Schneiderlin (kulia) ameitwa kuziba nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment