Wamiliki
wa mtandao wa kijamii wa Facebook ambao una watumiaji wengi zaidi
duniani wamelazimika kutoa maelezo juu ya kuondoka hewani kwa mtandao
huo kwa muda wa dakika 30 dunia nzima.
Msemaji wa Facebook amenukuliwa akisema kuwa “Mapema leo asubuhi
tulipata tatizo kubwa la watu kushindwa kuingia na kuandika chochote au
kupost picha katika mtandao wetu kwa muda wa dakika 30″
Anaendelea kwa kusema kuwa wametatua tatizo hilo haraka na kufanikiwa
kurejesha mtandao huo hewani kwa asilimia 100 ambapo pia ameomba radhi
kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Wakati mtandao huo ukiwa chini na watu kushindwa kupost wengi
walihamishia hasira zao kwa kuandika kupitia Twitter ambapo silimia 78
ya watu wanaotumia Facebook dunia nzima walishindwa kabisa kutumia
mtandao huo kwa dakika 30 wakati asilimia 21 ya watu waliweza kuingia.
Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment