Kiungo
wa Spain Cesc Fabregas (pichani) amefunguka leo kwa kusema alifanya
mazungumzo na kocha wa Arsenal Arsene Wenge kabla ya kuhamia Chelsea, na
kuambiwa kwamba nafasi yake tayari imeshacukuliwa na Mesut Ozil.
Fabregas alikuwa chagua la kwanza la Arsenal baada ya
mchezaji huyo alipoamua kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu uliopita,
lakini akamua kwenda Chelsea kwa dau la pauni milioni 30.
“Niliongea na Mzee Wenger naye akanambia atapata wakati mgumu kumpa nafasi ya kucheza kwani tayari Ozil alikuwa ameshachukua namba yangu”, Fabregas aliwaambia waandishi wa habari kwenye kambi ya Spain huko Brazil.
“Kulikuwa na timu kadhaa ambazo ningeweza kuchagua kwenda name nikachagua moja ya timu mbili ama tatu zilizo bora”, aliongezea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

“Nikaongea na Jose Mourinho naye akaongea mambo niliyotaka kusikia na mambo yakaendelea haraka haraka kuanzia hapo.
“Huu si muda muafaka wa kuongelea hayo, hata hivyo, kwani tunachohitaji ni kujali zaidi mambo ya timu ya taifa na kombe la dunia”, alisema.
Fabregas aliingia kipindi cha pili wakati Spain walipochapwa bao 5-1 na Holland katika mchezo wa kufungua dimba kwa kundi B.

Amesema yeye na wenzake wanatafuta hamasa kutoka mchezo
wao na Uswisi miaka minne iliyopita huko Afrika ya Kusini kwenye mechi
ya ufunguzi.
“Tunahitaji kufikiria ni jinsi gani tuliweza kuchuma katika miaka sita iliyopita,” alisema akimaanisha ushindi wa Spain katika michuano ya Ulaya kati ya miaka 2008 na 2012.

No comments:
Post a Comment