Kitengo
cha polisi cha Stockton, California kimezua mjadala mpya baada ya
kupost kwenye Facebook picha za mhalifu ili kipate msaada wa taarifa
zaidi za raia lakini kilichotokea na kuwa picha hiyo imewavutia zaidi
wanawake walibaki kuzungumzia uzuri wa mwanaume huyo.
Picha
ya mhalifu huyo aliyetajwa kwa jina la Jeremy Meeks (30) anayekabiliwa
na kiesi ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria imepata likes zaidi ya
66,000 na comments zaidi ya 20,000 kutokana na uzuri wa mhalifu huyo.
Jeremy
anatakiwa kutoa kiasi cha $900,000 kama dhamana yake kaisi ambacho kwa
kawaida ni kukubwa, lakini wanawake wengi waliocomment kwenye picha hiyo
wanazungumzia kuhusu kuchangia pesa ili wamtolee dhamana.
Wasichana wengine wametaka aachiwe ili wampe hifadhi nchini kwao, lakini kwa Meeks ni mtu wa familia mwenye mtoto mmoja.
Hata
hivyo, sura ya upole ya Jeremy na uzuri wake inaweza kuwa haiakisi
matendo yake kwa kuwa aliwahi kukaa jela miaka tisa kwa makosa ya jinai,
lakini pia ana alama ya chozi kwenye jicho lake la kushoto(drop tear)
inayoashiria kuwa alishawahi kufanya mauaji.
No comments:
Post a Comment