Rapa wa muziki wa nchini Marekani Wiz Khalifa
amedakwa na polisi katika uwanja wa ndege mjini Texas baada ya kukutwa
na kitu kinachodaiwa kuwa ni bangi wakati wa zoezi la ukaguzi ndani ya
mabegi yake.
Staa huyo anayetamba na ngoma yake ya “Black and Yellow” alikuwa akisafiri kutoka El Paso kwenda Dallas
wakati maafisa wa uwanja wa ndege walipokuta mzigo huo ndani ya begi
lake ambapo kwa mujibu wa sheria aliwekwa kizuizini na baadae kufikishwa
kituo cha polisi.
Lakini Rapa huyo hakuonyesha kujali na baadae alitweet picha yake akiwa jela kuonyesha hasumbuliwi na hatua ya kukamatwa kwake.
No comments:
Post a Comment