UGONJWA wa homa ya dengue yaani “dengue fever” umeingia jijini Mwanza ambapo mgonjwa wa kwanza ameripotiwa kulazwa hospitali ya mkoa, Sekou Toure. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Valentino Bangi amehibitisha kuingia ugojwa huo
ndani ya mkoa wake.
Ugonjwa huu ulithibitishwa kuingia nchini baada ya sampuli
zilizochukuliwa kutoka kwa watu waliohisiwa kuwa na ugonjwa huo jijini
Dar es Salaam kupelekwa kwenye maabara ya Taifa Dar es Salaam na
kuthibitisha kuwa na virusi vya homa ya dengue mwishoni mwa mwezi wa
Januari 2014.
Hadi sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na
ugonjwa huo ni 400 na vifo 3. Kwa wiki iliyoshia tarehe 9 Mei 2014 idadi
ya wagonjwa waliogundulika mkoani Dar es Salaam ni 60 (42-Kinondoni,
14-Temeke na 4-Ilala).
No comments:
Post a Comment