Taifa Stars na Malawi (Flames) zinapambana leo(Mei 27 mwaka huu) katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni.
Malawi tayari ipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi
hiyo wakati Taifa Stars iliyopiga kambi yake Tukuyu mkoani Mbeya
inawasili jijini Dar es Salaam kesho (Mei 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi
kwa ndege ya Air Tanzania.
Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Hiyo itakuwa ni mechi ya mwisho ya majaribio kwa Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kabla ya kwenda jijini
Harare kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika dhidi ya
Zimbabwe (Mighty Warriors).
Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani
Young Chidmozi nayo itakuwa inacheza mechi ya mwisho ya majaribio kabla
ya kwenda N’djamena kuikabili Chad.
No comments:
Post a Comment