Brazuca - mpira wa world cup |
Brazuca ndilo jina la mpira rasmi utakaotumika katika mchuano wa kombe la dunia Brazil hapo 12 mwezi ujao.
Watengenezaji Adidas pamoja na baadhi ya wachezaji wameusifu kwa shabaha na wepesi.
Brazil kwenyewe ndiko kuna wasiwasi - na Gwiji wa soka
nchini humo Pele anawahimiza raia wenzake warekebishe mambo. Balozi huyo
wa soka mwenye umri wa miaka 73 Ametiwa wasiwasi na maandamano ya mara
kwa mara ya kupinga matumizi ya hela nyingi za kuandaa kombe la dunia.
Maandamano hayo yameshangaza wengi kwani Brazil inahusudu na kusifika kwa ubingwa wao wa kusakata kandanda.
Ushauri
Pele anasihi maandamano hayo yakome kwani yatawafanya
wapenzi wa kandanda wa ng'ambo waliokuwa wanauia kwenda kujionea mchuano
huo kughairi.
Katika mkutano na waandishi habari huko Mexico amenukuliwa
kusema, ana taarifa kuwa tayari 25%ya mashabikii wa kigeni wameshavunja
safari zao za kwenda Brazil kwa sababu ya maandamano hayo na kama
yakiendelea basi wengine wengi huenda wakakata safari hizo na hivyo
kuleta hasara ya Brazil kukosa biashara hasa za kitalii.
Japo Pele anakubaliana nao katika maandamano hayo ya kutaka
kuboreshwa kwa huduma za kijamii hasa za matibabu, usafiri na elimu,
anasisitiza kuwa timu ya taifa ambayo imeiletea sifa tele nchi hiyo
isitumiwe kulipia makosa ya ufisadi unaofanywa na wanasiasa ambao
wanalaumiwa kwa maovu mengi ikiwemo kucheleweshwa kwa kukamilika kwa
viwanja 12 vya mpira , huku kukiwa zimesalia takriban wiki 3 tu kabla
kombe hilo kuanza.
Brazil ikiwa ndilo taifa lililoshinda kombe la dunia mara
nyingi kuliko lengine tena ugenini inakumbwa na shinikizo kubwa la
kushinda kombe hilo nyumbani.
Maandalizi
Kufikia sasa ni nchi chache tu ambazo tayari zimetaja
vikosi vyao ikiwemo hiyo Brazil na Uingereza, ambako, nahodha wa timu
hiyo Steven Gerald nae amekuwa akitathmini jinsi kikosi cha timu ya
taifa lake kilivyo na wachezaji chipukizi kiasi cha kuogofya.
Anasema anatumaini kuwa hawatashikwa na mchecheta wa uoga
watakapokuwa uwanjani Brazil. Majina yanayotajwa sana katika timu hiyo
ya Uingereza ni akina Ross Barkley, Raheem Sterling na Luke Shaw.
Nahodha Gerrard amewaomba wachezaji waliokomaa pamoja na yeye mwenyewe
wawashauri vyema vijana hao chipukizi watakapokuwa huko safarini
kutafuta ubingwa wa dunia katika soka.
Mechi ya kwanza ya Uingereza watakumbana na wa-italaino
hapo juni 15 katika uwanja ulioko eneo la msitu wa nyika ya Amazon
kunakojulikana kuwa na joto si haba.
No comments:
Post a Comment