Priince Charles na mkewe Camilla wakiwa katika ziara yao nchini Canada |
Naibu
balozi wa Urusi mjini London ameomba kukutana na maafisa wa wizara ya
mambo ya nje wa Uingereza kujadili matamshi ya Mwanamfalme wa Uingereza
Prince Charles ambapo amefananisha vitendo vya Rais wa Urusi Vladimir
Putin nchini Ukraine na uliokuwa utawala wa kinazi nchini Ujerumani
chini ya Adolf Hitler.
Prince Charles ambaye yuko kwenye foleni kumrithi Malkia wa
Uingereza , alitoa matamshi yake Jumatano alipokuwa anazungumza na
mfanyakazi mmoja wa Poland katika makavazi ya wahamiaji eneo la Nova
Scotia.
Walikuwa wanajadili hatua ya Hitler kunyakua nchi wakati wa
utawala wake wakati ambapo mwanamfalme huyo alipofananisha kitendo
hicho na kilichofanyika nchini Ukraine kwa maagizo ya Rais Vladimnir
Puti.
Prince Charles anatarajiwa kuhudhuria hafla moja nchini Ufaransa mwaka ujao.
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, amesema
kuwa sio jambo la kawaida mwanamfalme kutoa kauli za kisiasa wakati wa
mzungumzo ya faragha na kwamba kwa sasa hawawezi kutamka lolote kuhusu
zogo hilo.
Mnamo siku ya Jumatatu, Prince Charles na mkewe Camilla
walitembelea makavazi ya kitaifa ya wahamiaji nchini Canada, wakati wa
ziara yao ya siku nne nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema kuwa ombi la
kufanyika mkutano ni dalili ya Urusi kukasirishwa na matamshi ya Prince
Charles ingawa Urusi imejizuia kugeuza swala hilo na kulifanya kuwa
mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.
Inaaminika kuwa Urusi inataka ufafanuzi kuhusu matamshi ya Mwanamfalme huyo.
No comments:
Post a Comment