Masaa takribani 24 tangu alipotangazwa
rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal
amefunguka na kusema mwanafunzi wake na msaidizi wake wa zamani kwenye
klabu ya FC Barcelona Jose Mourinho ndio alikuwa mtu wa kwanza
kumpongeza kwa kupata Old Trafford.
Van Gaal mwenye
miaka 62 alitajwa rasmi kuwa mrithi wa David Moyes jana, na akiongea na
radio ya Uholanzi alisema kwamba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikuwa
mtu wa kwanza kumtumia message kumpongeza huku akimuambia kwamba
anamuonea wivu kwa kazi mpya na vilabu vingine alivyofundisha kama
Barcelona, Bayern Munich Ajax na timu ya taifa ya Holland.
Van Gaal anatarajiwa kuanza kazi United mara baada ya kombe la dunia...
No comments:
Post a Comment