Wapiganaji wa Al Shabaab
Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa maafisa wake wawili wa jeshi wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shaabab kufanya shambulio la kuvizia, baada magari yao kukwama barabarani huko Somalia.
Ripoti zinasema msafara wa wanajeshi wa Kenya ulikuwa ukielekea eneo la Ras Kamboni wakati shambulio hilo lilipotokea.
Kamanda wa polisi mjini Mombasa Robert Kitur amethibitishia bonifacemjailablog kuwa shambulio hilo limetokea.
Kwa upande wao, msemaji wa Al shabaab, Abu Mus'ab
amedai kuwa wapiganaji wake walifanikiwa kuteketeza magari kadhaa ya
jeshi la Kenya, madai ambayo yamekanushwa vikali na utawala nchini
kenya.
Aidha amesema wa wapiganaji kadhaa wa Al shabaab waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo.
No comments:
Post a Comment