Mlipuko
mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan katika Pwani
ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu mmoja kati
ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku wengine wanne
wakijeruhiwa vibaya.
Moto mkubwa
ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito wa tani 998
iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani ya maji baada
ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na majanga ya moto.
Watu saba
wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza majeraha ya moto
kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni wa meli hiyo
amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado unaendelea.
Afisa
usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo
bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa
wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati
mlipuko unatoke.
No comments:
Post a Comment