DAVID
LUIZ hii Leo alikuwa Jijini Paris akikamilisha taratibu zake za kuhamia
Paris Saint-Germain na akiwa huko alitoa salaam za shukrani kwa Klabu
yake Chelsea ambako kuna taarifa Mmiliki wa Klabu hiyo Roman Abramovich
ametoa idhini kuwa Dau la kumuuza Mbrazil huyo apewe Jose Mourinho
kununua Wachezaji wapya.
Huko Paris, Luiz amekuwa akipimwa Afya yake na kukamilisha Mazungumzo ya maafikiano ya malupulupu yake binafsi taratibu ambazo zinategemewa kukamilika hii Leo.
David Luiz ameuzwa kwa PSG kwa Dau la Pauni Milioni 50 zikimfanya awe ndie Beki wa Bei ghali Duniani na Fedha zote hizo zitakwenda kwa Jose Mourinho kununua Wachezaji wapya huku Straika wa Atletico Madrid, Diego Costa, ambae Mkataba wake una Kipengele cha kulipwa Dau la Pauni Milioni 31.5 ikiwa atauzwa wakati Mkataba wake haujaisha, akitajwa kuwa ni mmoja wa walengwa wakuu wa Mourinho.
Vilevile zipo taarifa zinamuhusisha Mourinho na Viungo Paul Pogba wa Juventus na Paulinho wa Tottenham.
Zipo kila dalili kuwa Mourinho anahaha kumpata Staa mkubwa kabla Fainali za Kombe la Dunia kuanza huko Brazil hapo Juni 12.
Akiongea na Jarida 'Globo Esporte.', David Luiz alituma ujumbe wa shukran ambapo alisema: “Asante Chelsea kwa Miaka 3 ½ ya uhusiano mzuri. Nimepata Marafiki, Mechi na Mataji ambayo daima yataishi kwenye fikra zangu! Nawashukuru Wafanyakazi, Wachezaji na Mashabiki” Luiz aliichezea Chelsea Mechi 143 tangu ahamie hapo kutoka Benfica ya Ureno.

No comments:
Post a Comment