Breaking News
recent

AMA KWELI UZEE MWISHO BUSATA, MJINI KILA MTU.....................

Babu Amos Makelle bada ya kufumwa akiwa na mfanyakazi wake gesti.
Chondechonde: Babu akiomba msamaha kutoka kwa makachero wa OFM.
Babu Amos Makelle baada ya kunaswa akiwa kitandani  na mfanyakazi wake aitwae Tina wakiwa tayari kuchepuka

Amakweli dunia imekwisha! Watu wa Dar es Salaam wanasema uzee mwisho Chalinze, Dar es Salaam kila mtu baby, kauli hiyo ilitimia usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita baada ya mmiliki wa Gesti ya GLP ya Mabibo Mwisho jijini Dar es Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku wa manane na mfanyakazi wake aitwae Tina.
Bosi huyo na mfanyakazi wake walinaswa na mchumba wa Tina aitwae Salum Mbonde ambaye alipenyezewa umbeya huyo na mteja mmoja aliyekodi chumba kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kufuatilia nyendo za wawili hao.
Baada ya mchumba wa Tina kupewa umbeya huo kuwa wawili hao walikuwa katika harakati za kuchepuka aliwawekea mtego na kuwashirikisha waandishi wa Oparesheni Fichua MaovuOFM na askari wa doria.
BOSI ATOA SHINGO KUCHUNGULIA NOMA
OFM na mchumba wa Tina wakiwa wamelizingira eneo la gesti hiyo mishale ya Saa 8:17 usiku kukiwa kumetulia tuliii... mtonyaji aliyekodi chumba kwa ajili ya kazi maalum aliwatumia ujumbe mapaparazi wa OFM kuwa mzee Makelle aliyekuwa kwenye chumba chake alitoa shingo kama mara tatu na kuangalia kulia na kushoto kama kulikuwa na mtu aliyemuona.
APIGA HATUA ZA KUNYATA
Ilipotimu saa 8:31, Mzee Makelle akiwa tumbo wazi na kipensi chake aliangalia tena kama hakukuwa na noma, akachomoka chumbani kwake fastafasta kwa hatua za minyato na kuzama chumba namba 104 alimokuwa Tina.
SHAAABASH... WANASWA KITANDANI
Shaaabash... baada ya dakika chache OFM na mchumba wa Tina walizama kwenye chumba hicho na kuwakuta wawili hao wakiwa kitandani huku Tina akiwa na nguo za ndani.
Walipohojiwa na OFM Tina alikuwa akilia na kumuomba radhi mchumba wake na kusema bosi wake huyo ndiye alimshawishi kuchepuka naye aliona kitendo cha kumnyima kingesababisha apoteze ajira yake ambayo anaitegemea.
Mzee Makelle alipohojiwa, katika hali ya kustaajabisha baada ya kujitetea alianza kumchongea Tina kwa mchumbaake akidai si mwaminifu.
“Wewe kama huyu ni mchumba wako hilo mimi nilikuwa silijui, lakini huyu mwanamke juzi tu kalala na mwanaume mwingine palepale gesti na kama unabisha twendeni nikawaoneshwe kitabu cha wageni muone jina lake na la huyo bwana,” alisema mzee huyo.
Waungwana waliokuwa wakimsikiliza mzee Makelle walimtafadhalisha kutozungumza maneno ya kichochezi na kumtaka ajitete mwenyewe.
Baada ya sakata hilo kijana huyo alimchukua mchumba wake na kuondoka naye ambapo OFM ilifuatilia na kubaini kuwa bado msichana huyo anaendelea kufanya kazi kwenye gesti hiyo.
Endapo mfanyakazi huyo atafukuzwa kazi na bosi wake baada ya kufumaniwa OFM inaiomba serikali kuingilia kati ili mwanamke huyo apate haki zake kwani bosi huyo awali alikuwa akisema huenda katika mchongo wa kumnasa Tina anahusika.
Credit: GPI
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.