HICHI NDICHO KILICHOMKUTA DAVIDO....
Anaitwa Davido Adeleke lakini kwenye muziki tunamjua kama Davido ambae labda tatizo linalomkuta Davido ndilo lilelile kama kwa Chris Brown na Justin Bieber yani kuwa na pesa nyingi na umaarufu vyote katika umri mdogo.
Akiwa kwenye harakati zake za kwenda kwenye show Uingereza Davido alifika airport na passport yake ya Marekani lakini maafisa wakamwambia alete passport ya Nigeria kwa sababu passport hiyo ya Marekani haikuwa na karatasi za visa ya kuingia Nigeria kwa hiyo utaratibu haujafuatwa.
Davido alisisitiza kwamba anayo passport ya Nigeria lakini ameiacha nyumbani hivyo hakuruhusiwa kusafiri hadi hiyo passport ya Nigeria ilivyoletwa ndio akaruhusiwa kusafiri kisha baada ya hapo ali-tweet akiwatukana maafisa wa airport kwa walichomfanyia.
Ofisi ya maafisa wa uhamiaji wamesema tabia kama hiyo ya Davido Adeleke sio sawa kabisa kwa sababu afisa huyo alifata utaratibu wa kazi ambao umemsaidia Davido ambae huko mbele ya safari angeweza kurudishwa au kuaibika zaidi kwani kwenye airport nyingine wako makini kwa hali ya juu kwenye vitu kama hivyo na wasingemruhusu kuendelea na safari.
No comments:
Post a Comment