Breaking News
recent

GOOGLE WAMETENGENEZA MAGARI YANAYOJIENDESHA, CHUKUA TIME YAKO KUYAONA.....

google
Kampuni ya Google inaanza kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe badala ya kuboresha vyombo vya moto vilivyotengezwa na makampuni mengine.
Magari hayo yatakuwa na vitufe vya kusimama na kujiendesha bila kuendeshwa na mtu,wala kuwa na usukani.
Picha za gari hilo zinaonyesha kuwa gari hilo ni kama mfano wa magarimengine ya mjini yenye muonekano mzuri, yaliyobuniwa kuyafanya yasitishe na kufanya watu wayakubali na kukubali teknolojia hiyo mpya.
google2
Mgunduzi msaidizi wa magari hayo, Sergey Brin amebainisha mipango hiyo jijini California.
Lakini pamoja na hatua hiyo, watafiti wanachunguza juu ya uwezekano wa kutumika kwa teknolojia hiyo mpya.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.