Breaking News
recent

JINSI JUVENTUS WALIVYOUSHANGILIA UBINGWA WA LIGI YAO... SERIE A..


May 18, 2014- huko Turin, Italia, Mabingwa Juventus wameweka Rekodi katika Ligi Kubwa Ulaya kwa kumaliza Msimu na na kuzoa Pinti 102 baada ya kuichapa Cagliari Bao 3-0.





Ingawa walikuwa tayari wameshatwaa Ubingwa, Juventus, chini ya Meneja Antonio Conte, waliingia kwenye Mechi hii na Cagliari wakiwa na ari kubwa ya ushindi na mapema tu Frikiki ya Andrea Pirlo ilimbabatiza Kipa Marco Silvestri na kutinga.
Kisha zikaja Bao za Fernando Llorente na Claudio Marchisio na kuifanya Juve, iliyokuwa ikicheza Uwanja wa Nyumbani, Juventus Stadium, iwe mbele 3-0 hadi Mapumziko.





Ushindi huu pia umeifanya Juventus  imalize Msimu ikiwa imeshinda Mechi zote 19 za Nyumbani za Ligi ya Italia…Pia Ushindi  ni wa 32 kwenye Serie A na kuwafanya wamalize Ligi wakiwa Pointi 17 mbele ya Timu ya Pili AS Roma.

Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.