Breaking News
recent

WENGER AELEZA KISA CHA UGOMVI WAKE NA MOURINHO, ASISITIZA WALA HAJUTII


Kocha Arsene Wenger amesema wala hatajuta kutokana na kitendo chake cha kumsukuma Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho.

Wenger alishikana na Mourinho wakati timu zao zilipokutana kwenye mechi ye Premier League kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na Arsenal ikalala kwa mabao 2-0.

“Nini cha kujuta, wala sitafanya hivyo. Nilikuwa ninatoka upande mmoja kwenda mwingine.
“Nilipogeuka nikakuta mtu yuko mbele yangu kabisa kanizuia.
“Halafu hasemi lolote, sasa unafikiri nitafanya nini,” alisema Wenger.
Mwamuzi wa akiba alilazimika kuingia kati kuwatenganisha makocha hao wasifikie kuchapana makonde.

Baadaye mwamuzi wa mchezo naye aliwaita na kutoa onyo kali akitishia kuwatoa uwanjani.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.