Raisi wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein ametumia kipengele cha sheria kinachomruhusu kumbadilisha Mwanasheria Mkuu na kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman.
Katika habari iliyotolewa muda mchache uliopita na Televisheni ya ITV ilisema nafasi ya mwanasheria huyo imechukuliwa na aliyekuwa msaidizi wake katika nasfasi hiyo Said Hassan Said.
Kabla ya kufukuzwa kazi mwanasheria huyo alitolewa katika Bunge la Katibauma lililopita kutokana na kitendo chake cha kukosoa rasimu ya tatu ya katiba, kitendo ambacho kilizua tafrani bungeni huku wabunge wengine wakimuita masaliti.
SOURCE: ITV
No comments:
Post a Comment